28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHIRIKA LA MAREKANI KUMSHTAKI TRUMP

NEW YORK, MAREKANI


Donald TrumpSHIRIKA moja la kisheria la Marekani, jana lilitarajia kufungua kesi mahakamani dhidi ya Rais Donald Trump.

Shirika hilo linamtuhumu kiongozi huyo kukiuka marufuku iliyowekwa kwenye katiba dhidi ya kupokea malipo kutoka Serikali za nje.

Kundi la mawakili na watafiti lilisema kuwa Trump amekuwa akipokea malipo kutoka Serikali za nje kupitia wageni kwenye hoteli zake na majumba yake ya kukodisha.

Walisema kuna kifungu kwenye sheria ya nchi hiyo ambacho kinaharamisha malipo kama hayo.

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Raia kwa ajili ya Wajibu na Maadili Washington (Crew), Noah Bookbinder alisema kuwa walitarajia Trump angechukua hatua ya kuzuia ukiukwaji wa katiba kabla ya kuingia madarakani.

“Hatukutaka kufika hapa. Matumaini yetu yalikuwa kwamba Rais Trump angechukua hatua zifaazo kuzuia kukiuka katiba kabla ya kuingia madarakani. Sasa tumelazimishwa kuchukua hatua za kisheria,” alisema Bookbinder.

Akizungumzia hatua hiyo, Eric Trump ambaye ni mtoto wa Donald Trump, aliielezea hatua hiyo kama ‘usumbufu tu kwa nia ya kufaidika kisiasa’.

Kwa mujibu wa New York Times, Eric ambaye ni makamu rais mtendaji wa shirika la Trump Organization linalomiliki na kusimamia biashara za rais huyo, alisema kampuni hiyo imechukua hatua kubwa kufuata sheria kuzuia kesi.

Alisema kampuni hiyo imeahidi kutoa faida kutoka katika hoteli zake, ambazo zimetokana na wageni kutoka Serikali za nje na kuziwasilisha kwa Hazina Kuu ya Marekani.

Katiba ya Marekani inasema hakuna ofisa yeyote wa Serikali anayepaswa kupokea zawadi au malipo yoyoye ya kifedha, au ada kutoka kwa Serikali ya kigeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles