24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Shindano la Hello Mr. Right! Msimu wa Sita laanza rasmi, vijana wahimizwa kufuatilia…

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shindano maarufu la kusaka wenza, Hello Mr. Right! msimu wa sita, limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam, likiwahimiza vijana kuzingatia fursa ya kujifunza namna bora ya kupata wenza wa maisha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Godfrey Lugalabam maarufu kama “Gara B,” alieleza kuwa msimu huu umeboreshwa kwa kuleta wakufunzi wapya, huku kaulimbiu ikiwa ni “Usione So!”

“Lengo la shindano hili ni kuwaunganisha watu wanaotafuta wenza, kuwapa mwongozo wa kutimiza ndoto zao za kujenga familia imara na yenye upendo,” alisema Gara B, akionyesha matumaini kuwa shindano hilo litaleta mwamko mpya miongoni mwa vijana.

Aliya Mohammed, mtangazaji wa kipindi cha Hello Mr. Right!, alifafanua kuwa shindano hilo litakuwa na washiriki wanawake 12, ambao watapata nafasi ya kusaka wenza wao wanaoamini kuwa ni “Mr. Right.” Aliya alisisitiza kuwa Hello Mr. Right! si shindano la kawaida, bali linazingatia maadili na kujenga msingi bora wa mahusiano.

“Shindano hili si la kiuni, linazingatia maadili yote ya kipekee,” alisema Aliya. “Washiriki watapewa mwongozo na ushirikiano wa kufikia viapo vya ndoa.”

Pia, Swalehe Nasoro maarufu kama “Dokta Kumbuka” alieleza kuwa atashiriki katika kutoa mafunzo kwa washiriki, akiwahimiza wanawake kutazama zaidi ya mwonekano wa nje au fedha wanapochagua wenza. “Mara nyingi wanawake hudanganyika na kuangalia muonekano wa nje au kipato. Mwanamume sahihi ana sifa za kipekee zaidi ya hizo,” alisema Dokta Kumbuka.

David Malisa, Meneja Masoko wa Startimes, alisisitiza kuwa msimu huu wa sita wa Hello Mr. Right! una ubora wa kipekee kama shindano la kwanza la Kiswahili lenye malengo ya kuwasaidia vijana kupata wenza. “Zaidi ya wanawake 450 na wanaume 800 wamejitokeza kushiriki shindano hili ili kupata wenza sahihi,” alieleza Malisa, akihimiza watu kufuatilia msimu huu bila kukosa.

Meneja Biashara wa St Bongo, Magreth, aliwahamasisha makampuni na wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ili kuimarisha zaidi. Naye Meneja wa Vipindi wa St Bongo, Raul Khan, alisema kipindi hicho kitakuwa hewani mara nne kwa wiki, kila Jumamosi, Jumapili, Jumanne na Jumatano, na kuwaahidi watazamaji zawadi na burudani kabambe.

Shindano la Hello Mr. Right! msimu wa sita linaahidi kuwapa vijana mwanga mpya wa kuchagua wenza sahihi na kujenga mahusiano yenye msingi madhubuti wa kifamilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles