24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHILOLE: PETE YANGU YA NDOA IMETOKA MAREKANI

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed “Shilole” amesema pete ya ndoa aliyovalishwa na mume wake, Ashrafu Uchebe, imetoka nchini Marekani.

Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu pete hiyo, Shilole alisema alipewa zawadi na mjomba wake kutoka nchini Marekani.

“Wanyamwezi tumefundwa, pete nzuri tumezawadiwa na mjomba wangu kutoka nchini Marekani,” alisema Shilole.

Mbali na kuelezea mahali alipopewa pete hiyo, msanii huyo aliwashukuru wasanii wenzake, Dogo Janja na Irene Uwoya ambao walimwahidi kumpa zawadi ya fedha na kugharamia filamu yake moja.

“Napenda kukupa zawadi yangu kupitia tasnia yetu ya filamu, andaa hadithi ambayo ina maudhui yoyote ya kuelimisha na kuburudisha, uniambie nitagharamia kila kitu,” alisema Uwoya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles