24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sheikh: Tuwapeleke watoto Madrasa kuwajenga kimaadili

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wazazi na Walezi ambao ni waamini na wasio waamini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wameshauriwa kuwapeleka  watoto  wao kwenye vyuo vya dini( MADRASA)ili waweze kujifunza maadili ya kidini na kupunguza mmomonyoko wa maadili ndani ya Jamii.

Wito  huo umetolewa na Shehe wa msikiti wa Ibaadh, Nuhu Mousa kwenye mashindano ya kusoma Qur’an yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Istiqaama yalikutanisha  vyuo mbalimbali vya madrasa  jijini hapa.

Mousa alisema ni vema walezi na wazazi kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto  wao masomo ya dini na ya dunia ili waweze kumtambua  Mwenyezi Mungu   kwani  kuishi bila dini ni sawa na mnyama.

Alisema  kila mzazi anawajibu wa kulea watoto wao kwa  kuwafundisha maadili ya dini  sanjari na kuwahamasisha  kupenda kusoma vitabu vya mwenyezi mungu pindi wanapotoka shuleni.

 “Inasikitisha kuona  mtu anaishi kama mnyama, kuna baadhi ya familia hawaoni umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kusoma mambo ya dini,  kufanya hivyo ni kosa, kila mzazi anawajibu wa kujitambua yeye ni nani  na kwa nini yupo duniani, ukujiuliza hivyo lazima utampeleka akajifunze dini yake,” alihimiza Mousa.

Kwa upande wake mwalimu wa madrasa ya Ilemela, Ibrahim Ramadhani alisema kuwa mtoto anapopata maadili ya dini anakuwa katika misingi bora wa kupata mwelekeo wa  familia yenye  nidhamu kwenye jamii.

“Mashindano haya yamekutanisha watoto 52  kutoka kwenye vyuo vya dini (madrasa), nane  vya jijini hapa kwani lengo letu ni kuhakikisha watoto wanatambua dini yao kwa undani zaidi kwa kuwa tunaimani  mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,”alisema  Ramadhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles