23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa SGR

Na Sheila Katikula, Mwanza

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya ujenzi wa reli ya mwendo kasi toka Mwanza kwenda Isaka mkoani Shinyanga itakaogharimu takribani Sh Trilion 3 na utatumia miezi 36  hadi kukamilika.

Wito huo umetolewa kwenye Kongamano la Mpango Kazi na Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya tano kutoka Mwanza kwenda Isaka uliokutanisha wadau mbalimbali jijini hapa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Masanja Kadogosa alisema makampuni yenye sifa yanatakiwa kuomba tenda za aina mbalimbali zinazohitajika kwenye Mradi huo haraka Ili kuepuka udanganyifu kwenye shughuli hiyo.

“Ujenzi wa sehemu ya Reli SGR toka Mwanza hadi Isaka utagharimu trilioni 3 na utakamilika ndani ya miezi 36 utasaida kuongeza huduma za usafiri kwa wananchi pamoja na bidhaa hivyo kusukuma gurudumu la maendeleo”alisema Mhandisi Kadogosa.

Mhandisi Kadogosa alisema kuwa Mradi huo utazalisha zabuni mbalimbali ikiwemo za usafirishaji, ukandarasi, na utatoa ajira kwa watu 15,000 za moja kwa moja na zisizo rasmi 75,000 na itakuwa na urefu wa kilometa 341.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. John Mongella, alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Mradi huo utasaida wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kutoka na kupeleka Daressalaam kwani zaidi asilimia 80 ya wafanyabiashara hutumia njia hiyo.

Mongella amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa zitakazoletwa na ujenzi wa Mradi huo kwani utazalisha uhitaji wa huduma nyingi toka kwa watanzania panapopita reli hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliwapongeza TRC kwa kuamua kuzishirikisha taasisi za fedha kuelekea kuanza kwa awamu ya tano ya ujenzi wa SGR kutoka mwanza hadi Isaka.

“Sote tunafahamu, CRDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo, hivyo tutahakikisha tunashiriki kwa njia mbalimbali katika ujenzi wa SGR ikiwemo kutoa mikopo kwa wakandarasi na kufadhili miradi mingine wakati wa ujenzi wa reli,” alisema Nsekela.

Alisema mpaka sasa benki ya CRDB imeweka sera wezeshi kwa wakandarasi ambapo inatoa dhamana ya Bid Guarantee kwa wakandarasi wanaotafuta kandarasi, dhamana ya utekelezaji  wa mradi inayofahamika kama Performance Guarantee na dhamana ya malipo ya awali yaani Advance Payment Guarantee.

Aliongeza katika kupanua uwigo wa huduma zake, CRDB itahakikisha inajenga matawi ama vituo vya kutolea huduma katika kila kituo kitakachojengwa na TRC kwenye njia ya SGR ili kuwaondolea usumbufu wasafiri wanapohitaji kutoa pesa.

Afisa Mahusiano wa Benki ya NBC Mwanza, Ester Kahabi amewataka wananchi kuchangamkia fursa za ujenzi wa kipande cha Reli hiyo kwa kuchukua mikopo yenye riba nafuu na kuwekeza katika Miradi ya ujenzi wa reli hiyo.

Aliongeza kusema kuwa Benki hiyo siku zote imekuwa bega kwa bega katika kuwezesha shughuli za Maendeleo ya nchini na kwa Sasa Benki inasaidia wateja kuchukua fedha kwa njia ya mtandao ya simu kwa haraka na kwa gharama ndogo za utoaji.

Kahabi aliwataka wakandarasi  wasambazaji na watoaji wa huduma hizo watumie Benki hiyo kupata mikopo Ili waweze kutoa huduma kwa ukamilifu katika kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles