25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa habari waahidi ushirikiano sekta binafsi

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wadau wa Sekta ya Habari wa Kanda ya Ziwa wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Waandishi wa habari nchini  ili kuifikisha taarifa zao kwa  jamii na kuihabarusha juu ya shughuli wanazofanya.

Hayo yanesemwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliondaliwa na klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kuelekea tukio la hafla ya usiku ya waandishi wa habari na wadau wa habari unaotarajia kufanyika Februari 1 mwaka huu.jijini Mwanza.

Ofisa Utekelezajikutoka Mfuko wa bima ya Afya (NHIF), Paul Bulolo, alisema waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa kufikisha taarifa kwa jamii zinazofanywa na  mfuko huo  na kupelekea wananchi kujiunga ili waweze kupata huduma pindi wanapougua.

Aidha Mkurugenzi wa shirika la Emedo, Editrudith Lukanga alisema ili kuweza kufikisha ujumbe kwa hadhira ni vema kila taasisi  kufanya kazi na waandishi wa habari ili kuweza kutimiza malengo yao kwa jamii.

“Naomba tuendelee kushirikiana ili tuweze kufikisha taarifa kwa jamii  ili kujua programu zinazowagusa wanawake na vijana nchini na kutatua changamoto zao,”alisema Lukanga.

Mkurugenzi wa Yuhoma Education Limited, Yussuph Yuhoma, alisema asilimia kubwa  ya Watu husoma vitu ambavyo  havipo sokoni na kupelekea kukosa ajira kwani kufeli mtihani siyo wa mwisho wa maisha.

Alisema Kampuni yake imejipanga kushirikiana na vyombo vya habari kuhamaisha kampeni hiyo ili kutoa elimu kwa jamii hasa vijana kuacha kukata tamaa pale wanapofeli mitihani ama usaili wa ajira.

Meneja Mauzo Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya TBL, Issa Makani  aliwapongeza MPC kwa umoja wao ulioanza na watu nane  na hivi sasa kuna wanachama  zaidi ya 130  na kusisitiza ofisi yao ilianza zamani kufanya kazi na waandishi wa habari hivyo inatambua umuhimu wao katika kufikisha ujumbe kwa hadhira. 

Mkuu wa kitengo cha mfuko wa bima ya afya kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando (BMC), Kelebe Luteli alisema kwenye sekta ya afya hospitali hiyo  imefanya mambo makubwa kupitia ushirikishwaji wa waandishi wa habari hivyo wataendelea kufanya kazi kwa karibu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko alisema wadau wa habari wasiviogope vyombo vya habari kwani waandishi wa habari siyo maadui  bali ni marafiki zao.

“Ni vema kuwepo na  ushirikiano baina ya wadau wa habari na vyombo vya habari ili kila mtu aweze kupata taarifa, ujembe kwa urahisi na wananchi kupata maendeleo,”alisema Soko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles