30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Shehena ya mirungi yakamatwa Kilimanjaro

Na Upendo Mosha,Moshi

Shehena ya dawa za kulevya aina mirungi zaidi ya kilo mia 400, misokoto ya bangi 1,401 zimekamatwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kuendeshwa kwa msako mkali.

Pia katika msakao huo,jeshi hilo limekamata jumla ya nyavu 180 zinazotumika katika uvuvi haramu katika bwawa la nyumba ya mungu.

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari, Jana Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwele, amesema operesheni hiyo ambayo imefanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa huo ikiwemo maeneo ya mpaka wa holili na Tarakea ilifanikisha kukamatwa kwa Dawa hizo.

“Tumekamata Shena za Dawa za kukevya aina ya mirungi, bangi pamoja na nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu pamoja na simu 238 zilizokuwa zinapitishwa kwa njia ya magendo katika mpaka wa Holili na Tarakea,”amesema.

Aidha, amesema katika operesheni hiyo askari walikamata pombe haramu aina ya gongo lita 223 na mitambo minne ,magari manne na pikipiki Tano zilizokuwa zinatumika kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Amesema katika operesheni hiyo jumla ya watu 59 wamekamatwa ikiwa Ni pamoja na pikipiki zilizokuwa zikitumika kusafirisha aina hizo za dawa za kulevya.

“Watuhumiwa wote tumewakamata na wapo chini ya ulinzi na upelelezi wa matukio yote ukikamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani na vyombo vyao walivyokuwa wakisafiria ambavyo ni magari mawili na pikipiki,”amesema.

Aidha, Kamanda Kamwele, alitoa wito kwa wananchi kufanya kazi halali za kuwaingizia kipato na kuacha mara moja tabia ya kujihusisha na biashara za magendo na haramu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles