20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Shebby: Rayvany, Kajala wasijisumbue picha haiwahusu

Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital

BAADA ya Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini, Shebby Love kutumiwa ujumbe mbalimbali ukimtaka kufuta picha ya mtoto wa muigizaji maarufu Bongo, Kajala Masanja ambaye ni Paula, ameweka wazi kuwa hamuogopi yoyote kwani hakuna kibaya alichokifanya.

Msanii Shebby Love

Akizungumza na Mtanzania Digital jana, Shebby amesema kuwa, alipigiwa simu na msanii Raymond Mwakyusa maarufu kwa jina la Rayvanny ambaye kwa sasa ni mchumba wa Paula akimuhoji kwanini amefanya hivyo lakini, amedai kuwa msimamo wake utabaki kama ilivyo na kwamba, hafuti hiyo picha kwani hamtambui kama ni mtoto wa Kajala.

“Baada ya kusambaa kwa ile ‘cover’ ya nyimbo yangu mpya ya ‘Kitu’ niliona simu ya Rayvanny akuiniambia kuwa, yuko bize na majukumu yake akimaliza atashuhulika na mimi kisa hiyo picha, mwingine ni Kajala aliyenipa masaa 24 niitoe lakini mpaka sasa sijaona akifanya chochote.

“Niseme tu picha iliyotumika mimi naitambua kama katuni na sio mtoto wa Kajala kwahiyo naendelea na muziki wangu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles