28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Shakira, J-Lo waisimamisha Super Bowl

Miami, Marekani

WAKONGWE wa muziki nchini Marekani, Shakira na Jennifer Lopez maarufu kwa jina la J-Lo, mwishoni mwa wiki iliopita waliacha gumzo kwenye mchezo wa Super Bowl LIV baada ya kufanya shoo ambayo iliwaacha mashabiki midomo wazi.

Wawili hao hawajawahi kufanya shoo ya pamoja kwa miaka mingi iliopita, hivyo wameandika historia kwa mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi.

Miongoni mwa mashabiki ambao waliguswa na shoo hiyo ni pamoja na mastaa kutoka familia ya Kardashian, Kim Kardashian na Kylie Jenner na Khloe Kardashian

“Ukweli ni kwamba wamewafunga watu midomo, hongera sana Shakira, J-Lo kwa shoo ya aina yake wakati wa SuperBowl Halftime.

“Umri na kile walichokifanya kimeshangaza wengi, walikuwa na nguvu kubwa, hakika wametushangaza,” alitwiti Kim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles