25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Sh bilioni 11 kutokomeza ukatili wa kijinsia

 Na MWANDISHI WETU -SHINYANGA 

MPANGO mkakati wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika Mkoa wa Shinyanga unatarajiwa kugharimu Sh bilioni 11. 

Mradi huo uliozinduliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack katika Kijiji na Kata ya Segese, Wilaya ya Kahama unakadiriwa kutekelezwa kwa mwaka mmoja. 

Lengo la mradi huo limeelezwa kuwa ni kuondoa ukatili na manyanyaso yanayowakabili wanawake na watoto na kuboresha hali za kundi hilo. 

Telack alisema mradi huo umetoholewa kutoka katika Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini Tanzania (Mtakuwwa) ambao ulianza mwaka 2017 hadi 2022. 

Alisema mpango wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Mkoa wa Shinyanga unatekelezwa kwa muungano wa mashirika ya kimataifa matatu na mawili ya hapa nchini. 

Kaimu Mratibu wa Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii nchini, Sifuni Msangi alisema mpango kazi huo ni kutokomeza vitendo vyote vya ukatili kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22. 

Msangi alisema mpango huo umekuwa shirikishi kuanzia ngazi ya taifa, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), NGOs, DPs na wadau wa maendeleo. 

“Pengine ndugu zangu niseme kuwa Serikali ilielekeza kuwa Tawala za Mikoa kuandaa na Serikali za Mitaa mipango mikakati midogo ya kutekeleza afua za Mtakuwwa kwa kuzingatia mahitaji ya mikoa husika” alisema Msangi. 

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais – Tamisemi, Dinah Atinda alisema uamuzi madhubuti kwa Mkoa wa Shinyanga kutekeleza mpango wa kuondoa ubaguzi na ukatili kwa wanawake na watoto uliodumu kwa vizazi na vizazi ni jambo ambalo likifanikiwa litaleta tija nchini. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles