27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi, walezi wakumbushwa kuwapatia watoto elimu ya dini

Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM 

 WAZAZI na walezi wametakiwa kuwahimiza watoto wao kupata elimu ya dini zaidi ili kuweza kuwajengea hofu na Mungu na kufata maadili mema. 

Akizungumza Dar es Salaam, wakati wa mahafali ya kuhitimu elimu ya Bibilia, Meneja wa Shule ya Hope Bible School, Mchungaji Bagoma Kise alisema wazazi na walezi wengi wamekuwa wakisisitizia watoto zaidi elimu ya kidunia kuliko ya Mungu kitu ambacho kinawasababishia mporomoko wa maadili katika maisha yao. 

Katika mahafali hayo jumla ya watoto 82 walihitimu ambapo katika ngazi ya awali wanafunzi walikuwa ni 57 na hatua ya pili 25. 

“Wazazi nawashauri wawasaidie watoto wao, ulimwengu wa leo kuna watu wamesoma elimu ya dunia, lakini hawana maadili, jiulize kwanini kuna rushwa, ufisaidi, uvivu, hii ni kutokana na kukosa maadili. 

“Mtoto anatakiwa kufundishwa hofu ya Mungu tangu akiwa mdogo ili akikua awe na hofu, na nawasihi sana wazazi wakati wanakazana sana watoto kupata alama nzuri ya elimu ya shule za kawaida, na pia wakazane watoto wao wapate mafundisho ya dini na kufanya vitu vizuri,” alisisitiza Mchungaji Kise. 

Alisema dunia ya sasa inahitaji watu kulifahamu zaidi neno la Mungu kutokana na uovu kuendelea kuongezeka siku hadi siku. 

“Tunaishi katika ulimwengu ambao watu wengi wametingwa sana, na kwa sababu hiyo wengine wanashindwa hata kwenda kanisani au sehemu ambazo semina za Bibilia zinafanyika. 

“Hivyo kupitia shule yetu ambayo inaendesha masomo haya kwa mfumo huria, inampatia mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika mahali popote kusoma na kujua Bibilia,” alieleza Mchungaji Kise. 

Alisema lengo lao ni kumsadia mtu kujifunza ili kuachana na uovu, hivyo kile ambacho mtu amejifunza aishi nacho. Alitoa wito kwa vijana kumtumikia Mungu wakati huu ambao wana nguvu na sio kusubiri kuwa wazee. 

“Vijana wengi wanadhani kuwa masuala ya kidini ni wazee, nawasihi sana vijana wenzangu kuwa wakati wa ujana ni wa kumtafuta Mungu na kumtumikia kwa sababu tunazo nguvu za kimwili na akili. Kama tutazitumia sasa hivi itatusaidia kulea familia na itawasaidia wakati wa uzee,” alisema Mchungaji Kise. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles