25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawekeza bil 1.8 kusaidia kilimo Simanjiro

Mohamed Hamad, Simanjiro



Serikali imetoa Sh bilioni 1.8 kusaidia kilimo cha umwagiliaji wilayani Simanjiro mkoani Manyara ili kuwakwamua wakulima kiuchumi.

Kutokana na hali hiyo, wilaya hiyo imetenga eneo lenye ukubwa wa heka 8,000 kwa ajili ya shughuli hiyo lengo likiwa ni kumkomboa mkulima kiuchumi kuondokana na umaskini wa kipato.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Yefred Myenzi amesema mbali na fedha hizo pia amepokea kiasi cha Sh milioni 300 kwa ajili ya upanuzi wa skimu ya umwagiliaji ya Ngage.

“Kilimo hicho kitakuwa ni cha uhakika kwani na maji yanayotumika yanatoka Ruvu hivyo atakayefanya kazi hiyo atakuwa na uhakika wa kilimo hicho,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula, ametoa wito kwa wawekezaji wa Kilimo kuja Wilayani humo kuwekeza.

“Niombe wawekezaji waje Simanjiro, mbali na aina mbalimbali za madini tuliyo nayo, pia kuna uwekezaji wa shughuli za kilimo, natamani waje hata sasa kuwekeza,” amesema.

Amesema Wilaya imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo ni fursa pekee kwao na kwamba atakayejisikia kuwekeza humo afike atapata maelekezo ya kina kufanya shughuli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles