24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Miaka 60 jela kwa kubaka, kumpa mimba mwanafunzi

Upendo Mosha – SihaMAHAKAMA ya Wilaya ya Siha imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 60, mkazi wa Kijijij cha Karansi wilayani humo,  Abrahamu Kaaya(23), baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Karansi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jasmine Abdul, alitoa hukumu hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi watano.

“Mahakama hii imemtia hatiani mshitakiwa Abrahamu Kaaya (23)  kutokana na kupatikana na makosa mawili,  la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 na ataenda kutumiki kifungo cha miaka 60 jela,”alieleza.

Alisema katika kosa la kwanza la ubakaji, mtuhumiwa amehukumia kifungo cha miaka 30  na kosa la pili la kumpa ujauzito mwanafunzi, amehukumia kifungo cha miaka 30 na  vifungo vyote vitaenda kwa pamoja.

Alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo haukuwa na shaka yeyote.

Hakimu alisema alitoa hukumu hiyo ili iwefundisho kwa watu wengi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo kama hivyo.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Simoni Feo, alidai  mshitakiwa alitenda kosa hilo Octobar 11 mwaka 2017  katika  Kijijiji cha Karansi.

Kabla ya kutolewa hukumu, mwendesha mashitaka aliomba mahakama  kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa kutokana na kukithiri   vitendo hivyo  iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles