24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa Sh bilioni 11 kuwezesha Wanawake na Vijana mkoani Dodoma

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

SERIKALI mkoani Dodoma imetoa mikopo ya Sh bilioni 11 kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi Novemba, 2021.

Hayo yaeelezwa Desemba 23, 2021 jijini Dodoma na Katibu Tawala Mkoa huo, Fatma Mganga wakati akiongea kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Uwekezaji wananchi kiuchumi kilichowashirikisha wanawake wajasiriamali, wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo.

Akieleza katika kikao hicho ameeleza fedha hizo zilizotolewa Katika Halmashauri za Bahi, Chamwino, Chemba, Dodoma Jiji, Kondoa, Kondoa mji, Kongwa na Mpwampwa ambapo Sh 7,004,724,612 zilielekezwa kwa wanawake, Sh 4,264,231,059 kwa vijana na Sh 652,795,298 kwa watu wenye ulemavu.

Ameleeza kuwa kutokana na fedha hizo miongoni mwa walionukaifa wanawake ni 12,427 na wanaume 2,249 na kueleza kuwa wanawake wameonyesha kuwa na ufanisi mkubwa katika kurejesha mikopo (43%) wakifuatiwa na wenye ulemavu (35%) na vijana (28%).

Ameeleza kuwa fedha hizo zimeelekezwa Kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vya machinjio ya kuku, kukamua mafuta ya alizeti, kusaga unga wa sembe, kutengeneza majiko banifu na mama lishe.

Pamoja na hayo amesema fedha hizo ambazo zimetolewa na serikali kwa vikundi vya wanawake, walemavu na vijana zimesaidia upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi ambayo hayawezi kukopesheka kupitia taasisi za kifedha ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanawake wanaojiunga na bima ya afya.

“Mikopo hii imeleta mafanikio makubwa katika uchumi wa wanawake, kwani wengi sasa wana ajira binafsi na hali ya maisha yao imeboreshwa kwa kuwa wanapata fedha za ziada kupitia biashara zao binafsi,” amesema Fatma.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia sekta za uchumi, Aziza Mumba ameeleza kuwa licha ya juhudi na mafanikio yaliyopo bado kuna upungufu wa rasilimali watu wenye weledi katika kusimamia utoaji na urejeshaji wa mikopo.

Ameongeza kuwa, kuna upungufu wa rasilimali fedha na vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa mikopo inayotolewa pamoja na idadi kubwa ya maombi ya mikopo ikilinganishwa na uwezo wa halmashauri husika jambo linalopaswa kushughulikiwa.

Akieleza tathmini ya utekelezaji sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Mkoa wa Dodoma, ameeleza kuwa ili kuondokana na kadhia hiyo kila Halmashauri zinapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ili kuongeza kiasi cha utoaji mikopo Kwa vikundi vya ujasiriamali vinavyoomba mkopo.

“Nashauri kuwepo na mafunzo ya uongezaji thamani ya mazao na kuunganishwa na mnyororo wa masoko kwa wanavikundi,ili kufanikisha hili lazima kuwepo na ubunifu wa mfumo wa Tehama ambao utasaidia kukumbusha waliokopa kurejesha fedha kwa muda na hatimaye kuwezesha wengine kukopa,” amesema Aziza.

Naye mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Tunu Pinda ametumia nafasi hiyo kueleza nafasi ya mwanamke katika uwekezaji kiuchumi ambapo amesema kutokana na wanawake wengi kuelimika na kukubali kujiingiza kufanya biashara hali zao za maisha zimeimarika .

Amesema, usawa wa kijinsia unaoendelezwa na serikali umesaidia kwa kiasi kikubwa wanawake kujitambua na kukubali kuwezeshana wao kwa wao na kuondokana na dhana ya udhaifu iliyokuwa imezoeleka.

“Wanawake wengi wanaishi kwenye nyumba nzuri, wanasomesha watoto, wanazingatia usalama wa chakula na yote haya yanakuja kutokana na faida ya uwekezaji, kwa ujumla tuko mbele sana kiuchumi kwa sasa asilimia 50 ya wanawake wanamiliki akaunti za benki,”ameleeza mama Pinda.

Mbali na hayo amewashauri wanawake kuendesha biashara zao Kwa kutumia mikopo kutoka taasisi za mikopo yenye riba nafuu hali itakayo wakwamua kiuchumi.

Amesema yeye binafsi amekiwa akikopa kwenye taasisi mbalimbali na kutumia fedha hizo kwenye masuala ya kilimo biashara na kusaidia kutoa ajira kwa wanawake wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles