24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mkandarasi Nico Andrew akabidhi madarasa kwa Meya Kumbilamoto

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amempongeza na kumshukuru Mkurugenzi wa Jecen Building Contractor Ltd, Nico Andrew, kwa kufanya ukarabati madarasa manne ya shule ya msingi Miembeni.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 23, 2021 wakati wa kukabidhiwa madara hayo Meya Kumbilamoto amesema Mkandarasi Nico Andrew amejitolea kufanya ukarabati huo kwa kutumia garama zake binafsi jambo ambalo si rahisi mtu kufanya.

“Tunampongeza ndugu yetu Mkandarasi Nico Andrew, kwa kufanya ukarabati wa madarasa haya kwa gharama zake, madarasa haya yamekamikika nimeona yametengenezwa kwa ustadi wa juu mchakato wa kumlipa fedha zake unaendekea,” amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wake Mkandarasi huyo amesema alikubali kuendesha mradi huo kwa fedha zake kwa sababu ni elimu ni jambo la msingi katika jamii hivyo ni vyema kuboresha mazingira ya kutolea.

“Ili mtoto aweze kupata elimu bora ni vizuri kutengenezea mazingira mazuri ndiyo maana siku sita kufanya mradi huu kwa sababu najua faida yake ni kubwa katika jamaii elimu inayotolewa leo hapa shuleni inaweza kubadilisha maisha ya Tanzania nzima,” amesema Andrew.

Ameongeza kwa kutoa wito kwa wadau wa makampuni na tasisi zisizo za kiserekali kujikita kuwekeza katika sekta hii ya elimu ili kutengeneza kizazi kilicho elimika na kuwa na wataalam wengi kama ilivyo nchi zengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles