24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi Bukoba washauriwa kuandikisha watoto elimu ya awali

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Wazazi na walezi katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameshauriwa kuwaandikisha watoto wao kujiunga na darasa la awali kwani ndio msingi wa mtoto kuimarika kiakili na kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamid Njovu wakati akizungumza na mwandishi wa Mtanzania Digital Ofini kwake mjini Bukoba, kuhusu mwamko wa wazazi na walezi katika uandikishaji wa watoto wenye umri wa kuanza darasa la awali.

“Ili kujenga msingi bora wa mtoto kielimu inatakiwa tuweke utaratibu bora katika elimu ya awali ili katika umri mdogo aingize vitu vitakavyo iandaa akili yake kwenda darasa la kwanza akiwa na ufahamu wa kutosha,” amesema Njovu.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Msingi, Baseki Sheja, amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka jana maoteo yao yalifanikiwa kwa asilimia 109 kwa waliojiunga na awali na wakati walioandikishwa darasa la kwanza walikuwa asilimia 112.28.

Amesema jumla ya watoto waliojiunga na madarasa ya awali ni 2,737 ambapo maoteo yao yalikuwa 2,500 ambapo kwa upande wa Serikali wavulana walikuwa 1,000 na wasichana 973, upande wa shule binafsi wavulana walikuwa 419 na wasichana 345.

Hata hivyo, Sheja amesema kuwa walioanza darasa la kwanza wavulana walikuwa 1,573 na wasichana 1,556 kwa shule za serikali wakati shule binafsi wavulana 411 na wasichana 390 jumla yake ni 3,930 na matokeo yao yalikuwa 3,500.

Aidha, Afisa elimu huyo amefafanua kuwa matokeo ya wanafunzi walioandikishwa mwaka mwaka wa masomo 2022 ni 4,027 ambapo wavulana ni 2,019 na wasichana ni 2,008.

Amesema kulingana na kipindi kifupi cha uandikishaji mpaka Desemba 20, mwaka huu wamesha andikishwa watoto 535.

“Idadi hiyo inakamilika kwa muunganiko ufuatao ambapo wavulana ambao tayari wameandikishwa ni 229 na wasichana ni 302 na wenye mahitaji maalumu wavulana ni 2 na wasichana 2 hiyo ni sawa na asilimia 26,” amesema.

Afisa huyo ameongeza kuwa maoteo yao kwa watoto wanaotarajia kuanza darasa la kwanza ni 4,202 ambapo wavulana ni 2,100 na wasichana 2,102

Mpaka kufikia Desemba 20, 2021 wameandikishwa wavulana 278 na wasichana 298 na wakati huohuo wenye mahitaji maalumu wavulana ni 6 na wasichana ni 3 hii inatengeneza jumla Kuu 585 ya walioandikishwa sawa na asilimia 28.

Anna Matayo mama wawa watoto watatu na mkazi wa Bukoba mjini amesema kuwa elimu ya awali kwa watoto wadogo imekuwa mkombozi kwa kuwaongezea uelewa na uchangamfu wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles