HARARE: Zimbabwe
SERIKALI ya Zimbabwe imesema itawashughulikia maveterani wa vita vya ukombozi nchini humo, wanaompinga Rais Robert Mugabe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Maveterani hao wanamwita Mugabe kuwa dikteta na msaliti ambaye amekuwa akiendesha nchi kwa ujanja ujanja huku akiacha matatizo ya uchumi yakizidi kuwa mabaya.
Pia wanampiga mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe,ambaye anaoneka kuwa nguvu kuliko Mugabe mwenye umri wa miaka 92.
Serikali ya Zimbabwe imekitaja kitendo cha maveterani hao kama cha usaliti, ikisema itawachukulia hatua wote waliohusika.
Maveterani hao wanadai Ris Mugabe ni dikteka aliyeuangusha uchumi wa Zimbabwe.
Kabla ya matukio ya sasa, maveterani hao walikuwa wakimuunga mkono Mugabe kwa dhati tangu nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru wake katika miaka ya 1970, na ndiyo waliomsaidia kushika madaraka nchini humo.
Hata hivyo, hivi aasa wanasema hawatamuunga mkono Mugabe ambaye anataka kuwania muhula mwingine wa urais mwaka 2018.
Limekuwapo ongezeko la maandamano ya kupinga utawala wa Mugabe katika siku za karibuni hasa kutokana na uchumi wa Zimbabwe kuendelea kodorora na kufikia kiwango cha serikali kushindwa kuwalipa mishahara wafanyikazi wake.
Chama cha Zimbabwe National Liberation War Veterans Association (ZNLWVA) kimemshutumu Mugabe kwa rushwa na matumizi mabaya ya fedha.