30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Zaidi ya taasisi 2000  yafungwa Uturuki ISTANBUL: Uturuki

 

Fethullah Gulen
Fethullah Gulen

SERIKALI ya Uturuki imesema imezifunga zaidi ya taasisi 2000 zenye uhusiano na kiongozi wa dini anayeishi  Marekani, Fethullah Gulen, ambaye anashitakiwa kwa kupanga mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa, Julai 15 mwaka huu.

Mashirika yaliyofungwa ni pamoja na vituo vya afya na zaidi ya shule binafsi 1000.

Serikali ya Uturuki inazituhumu  a taasisi hizo kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Gulen ambaye ana wafuasi wengi nchini humo.

Habari zinasema hatua hizo zimechukuliwa kama moja ya jitihada kubwa za kukabiliana na mitandao inayomuunga mkono   Gulen.

Gulen amekwisha kukanusha kuhusika na njama za mapinduzi ya  jeshi nchini humo yaliyosababisha vifo vya watu wapatao 246.

Maelfu ya wanajeshi, polisi na watu wengine wanaendelea kukamatwa nchini Uturuki kutokana na jaribio la  mapinduzi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles