26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

 Tim Kaine kuwa mgombea  mwenza wa urais wa Clinton

 Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama Democrat  katika Uchaguzi Mkuu wa Novemba mwaka huu,   Hillary Clinton (kulia) akimtambulisha mgombea mwenza wake, Tim Kaine (kushoto)
Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama Democrat katika Uchaguzi Mkuu wa Novemba mwaka huu, Hillary Clinton (kulia) akimtambulisha mgombea mwenza wake, Tim Kaine (kushoto)

WASHINGTON: Marekani

MGOMBEA urais wa Marekani kwa chama cha Democrat, Hillary Clinton amemtaja   senata wa zamani wa Virginia, Tim Kaine, kuwa mgombea mwenza  katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Kaine akiwa mwanasiasa mkongwe na mjumbe wa senate wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa,   Hillary anamuamini kuwa anaweza kumsaidia katika kupata ushindi dhidi ya mpizani wake Donald Trump wa chama cha Republican.

Hillary alitumia chaguo lake hilo njia ya ujumbe mfupi  katika mtandao wa jamii wa tweeter.

Habari zinasema Hillary aliamua kumteua  Kaine  (58) kwa vile ana sifa na historia nzuri.

Wengine ambao walionekana kama wangefaa katika nafasi hiyo ni   Waziri wa Kazi,  Thomas  Perez  na  Senata Cory Booker wa jimbo la New Jersey,    Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa kwanza kutafuta nafasi ya makamu  wa  rais.

Mwingine ni  James   Stavridis, mwanjeshi mstaafu  ambaye pia alikuwa kamanda wa kikosi cha majeshi ya Umoja wa Kujihami wa Nchi za  Ulaya Magharibi (NATO).

Kwa maelezo ya Hillay, yeye na Kaine   walikuwa wanasheria kabla hawajaingia kwenye siasa na walihitimu shule ya sheria katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Aliliambia shirika la habari la PBS  kuwa aliepuka kuchukua mtu mwenye uzoefu mdogo kama mgombea mwenza na pia hakutaka   kumtafuta mwanamke mwingine katika nafasi hiyo.

Baada ya Hillary kutangaza mgombea mwenza, timu ya kampeni ya Donald Trump, moja kwa moja ikadai kuwa Kaine ni mla rushwa na kuwa alipokea zawadi alipokuwa gavana wa Jimbo la Virginia.

Msemaji wa Trump, Jason Miller, alisema haina maana kwa Hillary kumteua mtu ambaye hana madili, kwa mujibuwa gazeti la   New York Times.

Trump amekwisha kumteua Gavana wa Jimbo la Indiana, Mike Pence kuwa mgombea mwenza wake katika Uchaguzi Mkuu wa Novemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles