25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 6, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatenga Sh bilioni 10 utekelezaji wa miradi ya maji

Upendo Mosha, Rombo

WAZIRI wa Maji, Juma Aweso, amesema Serikali imetoa zaidi ya Sh bilionI 10 za utekelezaji wa miradi mkubwa wa maji kwa mamlaka mpya ya maji na usafi wa mazingira wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati akiitangaza rasmi mamlaka hiyo na kuivunja kampuni ya utoaji wa huduma ya maji ya wilaya hiyo ya Kili Woter, alisema serikali imeamua kuanzisha mamlaka hiyo mpya ya maji kwa lengo la kuboresha huduma za maji kwa wananchi.

Alisema wilaya hiyo imepewa mamlaka kamili ya maji ili kusaidia kutatua kero na changamoto ya za upatikanaji wa majisafi na salama na kwamba jumla ya Sh bilioni 10, zimetolewa na serikali kwa mamlaka hiyo ili kuanzisha mradi mkubwa utakaosambaza maji wilaya nzima.

“Sijaja Rombo kuuza sura na kuondoka nimekuja kusaida wananchi wa Rombo kupata maji ya uhakika na badala ya kuwa na kampuni au bodi za maji sasa kuanzia leo Rombo mtakuwa na mamlaka yenu na niwatake sasa watendaji mfanyekazi na mbadilike mjue sasa hii Ni mamlaka ya maji…na kwakuanzia serikali inatoa bilioni 10 za mradi mkubwa wa maji.

“Namteua Martine Kinabo Kavishe,kuwa Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hii na nimshauri haakikishe anashikiana na watendaji na viongozi katika utendaji wake ili malengo tuliyonayo yafikiwe ..upo katika uangalizi kwa miezi mitatu ukiboronga tutakuondoa,”amesema.

Mbali na hilo aliutaka uongozi wa malaka hiyo kuanza majukumu yake mara moja kwa kifuata maadili, uamini na weledi mzuri katika kufanya kazi kwa kubadili mitazamo na kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ya maji.

“Kwenye taatifa nimesikia upotevu wa maji ni asilimia 60 ni nyingi mno, Mkurugenzi na timu yako mnayokazi ya ziada ya kufanya kudhibiti hili, panga timu yako na muhakikishe mnawajua wateja wenu na watendaji tunawapima mkileta uzembe hatutasita kuwaondoa,hamna taasisi inayojengwa kwa majungu shirikianeni,” alisema.

Katika hatua nyingine, Aweso amesema wizara hiyo imefanya maboresho mbalimbali katika utoaji wa huduma zake na kufikia makubalino ya kudhibiti wakandarasi wa miradi ya maji wanaoekeleza majukumu yao chini ya kiwango ikiwemo watendaji wazembe.

“Hatutokubali fedha za miradi ya maji ichezewe akibaina mtu tutamshughulikia ipasavyo, pia hatutakubali kuona wananchi wakibambikiwa Ankara za maji, na katika kupunguza changamoto hii wizara ipo kwenye mpango wa kununua mita za kisasa ili kuondoa changamoto ya ubambikiaji,”amesema.

Kwa upande wake aliyekuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya usambazaji wa maji ya Kili Woter,Prosper Kesi, alisema kampuni hiyo ilikuwa ikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upotevu wa maji kwa zaidi ya asilimia 60 jambo ambalo limekuwa likisababishwa na uchakavu wa miundombinu ya wateja.

“Kampuni imekuwa ikihudumia vijiji zaidi ya 60 vya wilaya ya Rombo lakini kutokana na changamoto mbalimbali tumekuwa tukishindwa kutoa huduma hiyo kwa saa 24 na badala yake tumekuwa tukitoa huduma hii kwa mgao,” alisema Aweso.

Alisema kampuni hiyo imekuwa ikishibdwa kujiendesha kutokana na baadhi yataasisi za serikali ikiwemo polisi na magereza kushindwa kulipa Deni la zaidi ya shilingi milioni 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles