22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Joshua ajinyakulia milioni 100 za SportPesa

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Droo ya Promosheni ya mwisho ya SportPesa iliyopewa jina la Mshiko Deilee imefanyika leo Jumanne Julai 13, 2021 na Joshua Sukambi (24) kutoka Kigamboni jijini Dar es Salaam amejishindia kitita cha Sh milioni 15.8.

Promosheni hiyo imefikia tamati leo baada ya kuchezeshwa kwa siku 30 ikishirikisha kampuni za Mitandao ya Simu ya TigoPesa, MPesa na Airtel Money.

Akizungumzia baada ya kupigiwa Simu na Wachezesha Droo hiyo, Joshua alianza kwa kushukuru baada ya ushindi huo na kusema kuwa “Najisikia freshi kabisa baada ya ushindi wangu, mimi ni kijana ninajishughulisha na biashara ya udereva wa bodaboda”.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas, amempongeza mshindi huyo na wengine waliokuwa wakishinda droo ndogo za siku na wiki akiamini pesa walizokuwa wanashinda zitabadili maisha yao.

“Leo tumefikia tamati ya promosheni yetu ya Mshiko Deilee yenye lengo la kuwatunza wachezaji wetu kila siku na wiki walikuwa wakipata zawadi na kutokana promosheni tuliyokuwa tunaiendelesha kwa kushirikiana na TigoPesa, Airtel Money na MPesa.

“Ninaamini Sh 15.8Mil inakwenda kubadilisha maisha ya Joshua ambaye ni dereva wa Bodaboda ambayo kama siyo yake, basi ninaamini atanunua yake na kuimiliki ili kusaidia familia yake.

“Kwa washindi wetu wa Sh milioni 100, 000, 000 wa kila wiki tunaamini zitawasaidia washindi wetu kuboresha ama kuanzisha biashara kwa mtaji huo ikiwa wanajishughulisha.

“Tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza na SportPesa ili na wao wajishindie pesa zitakazobadili maisha yao kama ilivyokuwa kwa huyu kijana aliyejishia Sh 15.8Mil ambazo ninaamini maisha yake yatabadilika kwake na ndugu waliomzunguka,”amesema Tarimba.

Kwa upande wa Muwakilishi kutoka Tigo, Fabian Felician ambaye ni Ofisa Huduma wa Kitengo cha TigoPesa alisema kuwa “Tunafurahia ushirikiano mzuri na SportPesa katika kuwezesha droo hii ambayo washindi wa kila siku, wiki na huyu wa mwisho, hivyo tunashukuru kwa kutuamini.

Meneja Biashara wa Airtel Money, Aggrey Charles alisema kuwa “Tunafurahia ushirikiano mzuri kati yetu na SportPesa ambao walituamini na kufanya kazi kwa pamoja na kumpata mshindi wa mwisho, hivyo tunawaomba wateja wetu kufanya mihamala yao kupitia Airtel Money.

Naye Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga amesema kuwa: “Tunawapongeza washindi wote kutoka SportPesa pamoja na huyu tuliyechezesha droo kubwa ya mwisho na kupatikana mshindi, pia niwapongeze SportPesa kwa kuchezesha droo yao kwa uwazi tukishirikiana na bodi hiyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles