32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATAKIWA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHUMA NCHINI

Na JOHANES RESPICHIUS

-DAR ES SALAAM

SERIKALI imetakiwa kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa za chuma nchini ili kulinda soko la ndani, kwani bidhaa ambazo zimekuwa zikiingia nyingi kati ya hizo zimekuwa hazina ubora wa kutosha, hivyo kuuzwa kwa bei ya chini na kuathiri viwanda vya ndani.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa uzalishaji wa bidhaa za chuma na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mshauri wa Maendeleo ya Viwanda kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa Japani (JICA), Hiroshi Kumagai, alisema uzalishaji wa chuma duniani umekuwa wa hali ya juu kuliko matumizi, hivyo nchi nyingi kukimbilia kuuza bidhaa zake nchini.

Alisema kutokana na uzalishaji wa chuma kuwa mkubwa, wawekezaji katika nchi husika wamekuwa wakiwezeshwa na serikali zao kutafuta masoko ambapo imefikia hatua ya kuifanya Tanzania kuwa dampo la bidhaa zisizokuwa na ubora.

“Uzalishaji wa chuma ni mkubwa kuliko matumizi ambapo nchi nyingi zinaingiza bidhaa zake nchini tena kwa bei ya chini baada ya sapoti kutoka serikali zao, jambo ambalo limekuwa linaathiri viwanda vya ndani,” alisema Kumagai.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Maganga Matitu Resource, Lawrence Manyama, alisema changamoto ambayo imekuwa ikikabili sekta hiyo ni upungufu wa wataalamu wazawa katika viwanda vya ndani.

Alisema hali hiyo imekuwa ikipelekea kulazimika kuleta wataalamu kutoka nchi za nje, kama vile China na India, ambazo zimepiga hatua kubwa kwa masuala hayo.

“Ukosefu wa wataalamu imekuwa changamoto kubwa kwa Serikali, hivyo inapaswa kuangalia upya mifumo ya vyuo vya ufundi ambavyo vimegeukia kuzalisha wahandisi, kuhakikisha vinazalisha mafundi mitambo wa kutosha.

“Kama kweli Serikali inalenga kufikia uchumi wa viwanda ianze utaratibu wa zamani wa vyuo vya ufundi kuzalisha mafundi mitambo, tofauti na ilivyo sasa mbapo vimegeukia kuwa vyuo vikuu kuto wahandisi. Hali hii ni sawa na kuzalisha madaktari bila kuwa na wauguzi,” alisema Manyama.

Aidha, aliishauri Serikali kushirikiana na JICA kuandaa mpango mkakati wa namna gani soko la Tanzania linaweza kukua likiwa na bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles