27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMISHI HOUSING YAWAPA MAKAZI WALIMU SITA DUGA

Na FERDNANDA MBAMILA

-DAR ES SALAAM   

KAMPUNI  ya  Watumishi Housing (WHC)  imekabidhi nyumba  sita  za  walimu wa Shule ya Sekondari Duga,  iliyopo Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, lengo ni  kuwasaidia kukabiliana na changamoto ya mazingira  magumu ya kufanyia kazi inayowakabili walimu nchini.

Akizungumza  na MTANZANIA hivi karibuni, wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Mkurugenzi  wa WHC, Mhandisi Lwitiko Mndobo, ambaye ni  Mkuu wa  kitengo cha  manunuzi, alisema lengo lao ni kuhakikisha  kuwa  watumishi  wa umma wanapata  nyumba  bora  ili waweze  kufanya  kazi  zao ipasavyo.

“Kama watekelezaji  wa mradi  huu  kwa kushirikiana na  Mamlaka ya Elimu (TEA), lengo  ni  kuhakikisha kuwa  tunajenga  nyumba  za bei  nafuu kwa  watumishi wa umma  na ndicho  ambacho  tumekuwa tukijitahidi  kuhakikisha kuwa tunasaidia serikali kupunguza nyumba za bei nafuu.

“Tunatambua kuwa mahitaji ya nyumba  za watumishi ni makubwa, hivyo  wito wetu ni kupata ushirikiano kwa mamlaka za wilaya zinazohusika  ili tuweze kujenga nyumba bora kwa watumishi kulingana na mahitaji na thamani  ya fedha,” alisema Mhandisi Mndobo.

Akipokea nyumba hizo kwa niaba ya Mkurugenzi, Ofisa  Elimu wa  Wilaya ya Mkinga,  Omary Kombo, alisema  nyumba hizo zitawasaidia walimu kuondokana na adha ya  kuishi  mbali na shule.

“Tumepokea vyema  nyumba hizi,  tunaamini kukamilika  kwake zitakuwa na uwezo wa  kuchukua walimu  sita na hivyo  itaondoa adha  za walimu wetu  wanaopanga mitaani  na kusaidia kuongeza hadhi ya juu kwa walimu.

 “Ni wazi kuwa  serikali  yetu  sasa hivi  inawathamini  walimu  wake, kwani hakuna aliyetegemea kuwa  tungepata  nyumba hizi katika  miaka  ya hivi karibuni,  pia ni nyumba  ambazo zimechukua muda,  ikilinganishwa na nyingine zinazojengwa na wakandarasi  wa ndani, hivyo  tunawashukuru WHC na TEA na sisi tumezipokea  na tutazilinda,” alisema Kombo.

Upande wake, ofisa rasilimali  watu  kutoka TEA, Richard  Chiteji, alisema kwa sasa wanatekeleza miradi  mbalimbali  kwenye wilaya 40 ambapo kila shule itakuwa na nyumba moja  yenye  uwezo wa kupokea  walimu  sita, huku akiwataka wanufaika wa mradi  huo kuzitunza nyumba hizo ili kuwa mfano kwa taasisi  nyingine kupitia mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles