24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yataja wanaotakiwa kupata chanjo ya homa ya ini

Ramadhan Hassan -Dodoma

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema si wananchi wote wanapaswa kupata chanjo ya homa ya ini (Hepatitis B).

Imesema walio katika hatari zaidi ya kupata maambukizi hayo ndio watakaopatiwa chanjo kwa utaratibu wa kuchangia gharama.

Wizara hiyo ilitoa kauli hiyo jijini hapa jana wakati ikijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Taska Mbogo (CCM).

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua mpango wa Serikali wa kutoa chanjo hiyo kwa Watanzania ambao hawajaipata kwani ugonjwa huo ni hatari.

Alisema Serikali imekuwa ikitoa chanjo ya Hepatitis B kwa watoto wote kupitia chanjo ya pentavalent yenye mchanganyiko wa chanjo za dondakoo, kifaduro, pepopunda, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo  kuanzia mwaka 2002 na hivyo kuhakikisha wananchi wote waliopata chanjo hiyo wakiwa wachanga wamekingwa.

Ikijibu swali hilo, wizara ilisema kwa wananchi wengine ambao wamezaliwa kabla ya mwaka 2002 na hivyo kutokupata chanjo hiyo, Serikali imekwishaainisha makundi maalumu ambayo yatapatiwa chanjo hiyo kwa kuchangia gharama.

Ilisema  utaratibu huo utafanyika kwa awamu, kwa kuanzia kwenye hospitali za rufaa za mikoa na baadaye hospitali za halmashauri ili wananchi wenye uhitaji ambao wapo katika makundi yaliyoainishwa wapatiwe chanjo kwa kuchangia gharama kwa kiwango kitakachowekwa na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles