29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasisitiza ujenzi Bandari ya Mwambani

Samuel-Sitta1NA OSCAR ASSENGA
SERIKALI imesema mpango wa ujenzi wa bandari mpya ya Mwambani mkoani Tanga upo kama ulivyopangwa.
Kujengwa kwa bandari hiyo, imeelezwa itakuwa ni kichocheo cha mabadiliko ya kiuchumi ndani ya Mkoa wa Tanga ambapo shehena za mizigo zitaongezeka mara dufu kuliko ilivyo sasa.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mkoa wa Tanga katika ziara yake ya kikazi ya kukagua bandari hiyo na eneo linalotakiwa kujengwa bandari mpya ya Mwambani.
Sitta alisema mradi huo wa bandari mpya unakwenda sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara kutoka Pangani, Bagamoyo hadi Dar es Salaam pamoja na njia ya reli ya kutoka Tanga- Arusha, Musoma hadi mikoa ya Kanda ya Ziwa kuelekea Uganda.
Alisema tayari Serikali imeshaliagiza Shirika la Rasilimali za Reli (Rahco) kuhakikisha inajenga kituo kikubwa cha kugeuzia treni na mabehewa.
“Rais Museven wa Uganda alitoa rai kwa Rais Jakaya Kikwete kujenga reli itakayokwamua uchumi wa Uganda na ukitazama ramani ya Afrika hususan Afrika Mashariki Bandari ya Tanga ndiyo njia fupi karibu kabisa kwa kuweza kusafirisha bidhaa za Jamhuri ya Uganda,” alisema Waziri huyo.
Sitta alisema fursa hiyo inachangiwa pia na ugunduzi wa madini aina ya Red Nicol katika Mkoa wa Simiyu eneo la Dutwa pamoja na Soda Arsh katika Ziwa Natron, rasilimali ambazo zote zinatafutwa duniani na zitasafirishwa kwa njia ya reli kupitia Tanga kuelekea kwenye soko la kimataifa.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, mradi huo wa njia ya reli unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 4 sawa na Sh trilioni 8 na utafanyika chini ya mkandarasi Kampuni ya China Engineering ambaye atajenga kwa gharama zake mwenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles