22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa tuhuma za utapeli

Na Upendo Mosha
SERIKALI wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, inamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Preygod Mmasi, kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli kwa kutumia kivuli cha Ofisi ya Waziri Mkuu na kuwatapeli wawekezaji wilayani humo kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Serikali.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo, Athoniy Mtaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani humo, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni mosi mwaka huu saa 3 usiku mkoani Arusha akijiandaa kukimbia.
Mtaka alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulifuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuwa yupo mtu anayejitambulisha kuwa ni mkurugenzi wa taasisi iitwayo JOFA, akidai kuwa amepewa kibali cha kufanya kazi ya kampeni za adhari za mazingira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).
“Katika zoezi hilo walifika katika maeneo ya wawekezaji kama vile barua inavyoeleza lakini ndani ya zoezi hilo walitoza watu faini katika makundi mbalimbali ya watu na viwango mbalimbali vya fedha bila risiti na nilipata malalamiko hayo kwa mmoja wa wahanga na kufuatilia suala hili na kubaini kuwa kuna harufu ya utapeli,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles