23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAPIGA ‘STOP’ MWALO WA KIRANDO

Na Gurian Adolf-Nkas


SERIKALI mkoani Rukwa, imepiga marufuku kuutumia mwalo uliopo katika Kijiji cha Kirando Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushusha mizigo, kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki.

Mkuu wa mkoa huo, Joachim Wangabo, alisema hayo jana wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Nkasi na kukuta mwalo wa Kirando unatumika kama bandari, ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafirisha  kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika.

Alisema wananchi wasipotoshe lengo la kutengwa kwa  mwalo huo ambayo ni kwa ajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye Ziwa Tanganyika na si kwa ajili ya magari ya kupakilia mizigo.

“Lengo la mwalo huu ni kuuzia samaki na dagaa, lakini naona mizigo hii imegeuzwa kuwa bandari, narudia ni marufuku kupakia mizigo katika mwalo huu kwani hapa ni  sehemu ya kuuzia mazao yatokanayo na ziwa na si vinginevyo,” alisema Wangabo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri, hivyo ni lazima iboreshwe ilirudi kama ilivyokuwa awali.

Awali Mbunge wa Nkasi Kaskazini,  Ally Kessy (CCM), alikemea vitendo vya wananchi wa Kirando kutumia mwalo huo kama bandari, jambo ambalo ni kinyume na sheria na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.

“Nawaomba ndugu zangu kuanzia sasa hii si bandari na haipo chini ya TPA, bandari ni ile ya zamani na iendelee kutumika ile ile na hapa tuwaachie wavuvi,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda, aliwaasa wananchi wanaotumia vyombo usafiri ziwani kuzingatia kuvaa maboya na kuonya kutozidisha mizigo na abiria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles