28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga marufuku maandamano mapya Nigeria

Abuja, Nigeria

Waziri wa Habari wa Nigeria, Lai Mohammed ameonya dhidi maandamano yaliyopangwa kufanyika huko Lekki jijini Lagos ambapo vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waaandamanaji Oktoba, mwaka jana.

Maandamano mapya, yaliyopewa jina la ‘Occupy Lekki toll gate’, yamepangwa kufanywa Jumamosi Waandaaji wanasema watagomea dhidi ya kufunguliwa tena kwa lango la ushuru.

Mohammed amesema serikali haitaruhusu maandamano mengine kufanyika.

Alisema wahalifu wanaweza kuvamia maandamano na kusababisha watu kupoteza maisha na uharibifu wa mali.

Amesema matangazo ya kuwataka watu kujitokeza kwenye maandamano yamekuwa yakisambazwa

Waziri aliongeza kuwa serikali ilikubaliana na matakwa ya awali na kuachiwa kwa waandamanaji waliokuwa wamekamatwa wakati wa wimbi la kwanza la maandamano na kuunda tume huru kutazama suala la ukatili wa polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles