23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuleta mswaada mabadiliko sheria ya ndoa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Taasisi ya Msichana Initiative na wadau mbalimbali wanaotetea haki za wanawake wameiomba Serikali kupitia bunge kuleta mswaada wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kulinda haki za mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni

Akizungumza wakati wa mkutanonhuo leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Ininiative, Rebeca Gyumi, amesema lengo la Mkutano huo ni kujadili namna bora ya kuunganisha nguvu za pamoja ili kuishawishi Serikali.

“Kwa pamoja tukishawishi Serikali kupitia bunge ili kuleta mswaada wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kulinda haki za mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni kwani kuna mkanganyiko katika sheria ya mtoto na sheria ya ndoa.

“Mkanganyiko uliopo ni kwamba sheria ya mtoto imebainisha kuwa mtoto ni mtu yoyote mwenye umri chini ya miaka 18 wakati sheria ya ndoa inaruhusu msichsna wa miaka 14 kuolewa jambo ambalo unaonesha mtoto wa kike chini ya miaka 18 anaruhusiwa kuolewa kisheria.” amesema Rebeca

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi, amesema mchakato wa mabadiliko ya sheria ya ndoa unahitaji nguvu za pamoja ili kulinda haki za mtoto wa kike hivyo amezitaka Taasisi na asasi za kiraia kushiriki mchakato huo ili kuzuwia mimba za utotoni.

Naye Nuria Mshale kutoka Shirika la save the Children amesema ni jukumu la kila mtu kwa nafasi yake ikiwemo Wabunge kupiga vita uwepo wa sheria ya ndoa inayoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kuolewa kwani inamkosesha haki nyingi mtoto wa kike.

Katika Mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es salaam na kukutanisha zaidi ya mashirika 70 na asasi mbalimbali zinazoshughulikia haki za wanawake ikiwemo Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Chama cha wanasheria wanawake TAWLA pamoja na Save the Children ili kujadili changamoto za sheria ya ndoa huku lengo likiwa ni kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles