27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yanunua Tanzanite ya Bilioni 2.24

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite,Anselm Kawishe,sasa ni bilionea mpya mjini hapa baada ya kusota miaka 15 akichimba madini hayo na kufanikiwa kupata vipande viwili vya madini vyenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 2.24.

Leo Agosti 27,2022,Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Nduguru amemtangaza bilionea huyo katika eneo la mji mdogo wa Mirerani,wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

Amesema Kawishe amepata vipande viwili vya madini ya Tanzanite ambapo kipande cha kwanza kina uzito wa kilo 1.48 kikiwa na rangi na ubora wa hali ya juu huku thamani yake ikiwa Sh Milioni 713.8.

Amesema kipande cha pili kina ukubwa wa kilo 3.74 kikiwa na uzuri na ubora wa kati huku thamani yake ikiwa Sh Bilioni 1.5.

Kutokana na unyeti wa suala hilo, Waziri wa Madini, Doto Biteko,amesema mawe yote hayo yamenunuliwa na Serikali na yatahifadhiwa kama hazina ya taifa.

Mbali na Biteko,tukio hilo lilihudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, watendaji wengine pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wa madini nchini.

Biteko akizungumza kabla ya kumkabidhi Laizer mfano wa hundi ya thamani ya Sh bilioni 2.2 alimpongeza kwa kukubali kuwa mzalendo na kuuza serikalini madini hayo kwa kuwa huo ni ushahidi kuwa hata wachimbaji wadogo wanaweza.

Amesema uamuzi wa kuuza madini hayo umefanywa na Kawishe mwenye kwa kuwa na imani na Serikali yake na sio vinginevyo na kuwataka wachimbaji wadogo wa madini kuongeza juhudi katika shughuli zao ili idadi ya mabilionea iweze kuongezeka.

Amesema baada ya kukubaliana na mchimbaji huyo,serikali iliamua kuyanunua ili yawekwe kwenye makumbusho ili kuidhihirisha dunia kuwa Tanzania ndiyo kitovu cha madini hayo badala ya kuuzia mataifa mengine na kupeleka kwenye maonyesho yao.

Aidha amesema ujenzi wa kituo cha Tanzanite City kinachojengwa katika mji huo kitasaidia kunufaisha wafanyabiashara na wa madini hayo lengo likiwa ni kutaka madini hayo kuuzwa katika mjii wa Mirerani ili kunufaisha wananchi na wachimbaji hao.

Amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani makusanya ya kodi ya Serikali Kwa Madini ya Tanzanite yameongezeka kutoka Sh Bilioni 475 hadi Sh Bilioni 625 Kwa Mwaka na hayo ni matanikio makubwa katika sekta ya Madini ya Tanzanite.

Waziri Biteko alisema sekta ya Madini imepanda katika ukusanyaji kutoka asilimia tano hadi kufika asilimia Saba na kufanya uuzwaji wa Madini nje ya nchi kuwa Mzuri na Wenye tija Kwa serikali.

Naye Bilionea Kawishe akizungumza bàada ya kusaini mkataba wa mauziano na Serikali amesema amechimba kwa zaidi ya miaka 15 bila mafanikio.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka,amesema amempongeza Kawishe kwa kufanikiwa kupata madini hayo, huku akiomba serikali kurekebisha barabara ya kutoka geti la Magufuli hadi lami kwa kuijenga kwa kiwango cha lami huku barabara ya ndani kuelekea kwenye migodi kuomba ijengwe kwa njia kiwango cha moramu.

“Hata mimi nisipokuwa bilionea, wananchi wangu wakiwa mabilionea ndiyo namimi nafarijika, tumezidi kuzalisha mabilionea wapya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles