25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ubungo yaanza kudhibiti ukatili

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam imenza mkakati wa kudhibiti vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto huku ikianza na maeneo hatarishi.

Lengo la mkakati huo ni kuhakikisha kuwa wanadhibiti matukio yote ya ukatili ambapo wataanza na kata nne za Manzese, Mabibo, Mburahati na Makurumla ambazo ndizo zinaongoza kwa matukio ya ukatili ukiwamo wa kijinsia.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la Usawa wa Jinsia Tanzania, Msafiri Mariam ambapo amesema kuwa lengo ni kufikia mkoa mzima wa Dar es Salaam.

“Lengo la kuitisha viongozi wa mtaa, watendaji kata, polisi kata, viongozi wa dini na makundi ya kijamii ni kutaka kutoa elimu ya pamoja na kubadilishana uzoezi namna ya kupambana na vitendo vinavyotokea.

“Tumechagua kata hizo nne kwa kuwa ndizo zinaongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia pia kwenda kuwahamasisha watendaji hawa kwenda kuibu vitendo vya ukatili kwa kuunda kamati za mpango mkakati wa serikali wa kutokomeza ukatili(MTAKUWWA),” amesema Msafiri.

Akizungumzia aina ya ukatili unaoongoza Msafiri amesema kuwa ni ukatili wa kingono unaohusisha ubakaji na ulawiti kwa watoto waadogo hasa wa shule ya msingi.

“Kila siku tunakazi ya kuokoa watoto ndiyo maana utaona kwamba kuna maeneo hatarishi ambayo tunayatazama mitaa kama uwanja wa fisi, shidere na manzese ni sehehemu ambazo zimakuwa siyo salama kwa watoto.

“Pia kuna kukithili kwa rushwa ya ngono kwa wafanyakazi wa ndani ambapo kila siku tumekuwa na kazi ya kutoa msaada na ndiyo sababu tumekuja na mkakati huu,” amesema Msafiri.

Awali, Baadhi ya washiriki wa mkutano huo akiwamo Mwenyekiti wa Mtaa wa Chakula Bora, Oddo Ramadhani amesema kuwa elimu inahitajika ili kukomesha ukatili wa kijinsia kwani kumekuwa na matukio mengi yakiwamo ya wanawake kutelekezwa na wenzi wao sambamba na ubakaji.

“Wanawake wanapigwa sana na wanaume zao, lakini pia watoto wa kike wanabakwa sana, hivyo kwa elimu hii tutaenda kuwaelimuisha wananchi na wataelewa madhara yake,” amesema Oddo.

Sheikh wa Kata ya Manzese, Haji Mohamed amesema kuwa ukatili ni kitu kisichokubalina na kinatakiwa kupingwa kwa nguvu zote.

“Elimu hii nitakayoipata hapa nitaenda kuitumia kwenye mawaidha yetu ili kutoa elimu kwa wananchi kujua athari za matendo hayo, kwani tunataka kuwa na jamii salama,” amesema Mohamed.

Upande wake Editha Ibrahim ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Mburahati amesema changamotyo kubwa bado ni upande wa wanawake ambao wamekuwa wakikosa ujasiri wa kujitokeza kuripoti matukio ya ukatili jambo ambalo linachovhea kuzalisha jamii isiyo na maadili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles