29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali yakusanya Sh trilioni 1 kwa mwezi

likwelileNa Mwandishi Wetu, Dar es salaam

SERIKALI imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh trilioni 1 kwa mwezi huu, tofauti na Sh bilioni 850 zilizokuwa zikikusanywa kwa mwezi hapo awali na kuzielekeza fedha hizo katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile, wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa Sh bilioni 18.7  kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada, chakula pamoja na ruzuku.

Dk. Likwelile, alisema Mkoa wa Dar es salaam  umeongezewa Sh bilioni mbili ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais Magufuli, alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao , wizara imetoa Sh bilioni 1.65  kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo  wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, huku walimu walio masomoni wametengewa  Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.

“Fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya  mishahara ya watumishi wa umma,  ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi ya jamii zimetolewa Sh bilioni 81.13.

“Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi bilioni 23.078, mpango wa maji vijijini Bilioni l7.1, maendeleo ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini zimetengwa shilingi  bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama imepatiwa shilingi bilioni 12.3,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles