31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi DRC akaribishwa kwa maombi Dar

jeanNa Elias Msuya, Dar es Salaam

JUMUIYA mbalimbali za raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waishio jijini Dar es Salaam, jana walikusanyika katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo maeneo ya Upanga kumkaribisha Balozi mpya, Jean Mutamba, huku wakimwomba atatue kero zao.

Balozi Mutamba anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Juma Mpango aliyemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka jana, alikwenda Ikulu kuwasilisha nyaraka zake kwa Rais Dk. John Magufuli kabla ya kufika katika ofisi za ubalozi huo jana saa nne asubuhi.

Awali akizungumza kabla ya kumwombea balozi huyo, Mchungaji David Paul wa Kanisa la Elishadai Kingdom, alisema kiongozi yeyote hutolewa na Mungu, hivyo Balozi Mutamba ameletwa na Mungu kuwasaidia Wakongo waliopo Tanzania.

Katika hafla hiyo, mchungaji huyo aliungana na jumuia mbalimbali za wakongo kusali kwa pamoja sala ya kumwombea balozi huyo kwa lugha ya Kifaransa.

“Tunajua kila kiongozi hutoka kwa Bwana na wewe umetoka kwa Bwana, atakujalia busara kama alivyofanya kwa mfalme Suleiman kwa sababu Mungu habadiliki, ni yule yule jana na leo hata milele,” alisema Mchungaji Paul.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, Godefroid Kabobo alisema ujio wa balozi huyo unafungua ukurasa mpya wa kibishara baina ya nchi hizo mbili.

“Hii ni mara yetu ya kwanza kukusanyika kama hivi katika ubalozi wetu. Tunaamini kuwa hii ni dalili njema itakayotufungulia milango ya kibiashara.  Tuna changamoto nyingi za kibiashara ambazo ni mizigo yetu kuchelewa bandarini lakini pia malipo ya kuhifadhia mizigo ni makubwa mno,” alisema Godefroid.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Wakongo waishio Tanzania, Jean Lopenge alitaja moja ya kero zao kubwa kuwa ni hati za kusafiria na ruhusa za ukaazi (working permit).

“Tuna shida ya viza imepanda bei pamoja na ruhusa ya ukaazi, inatusumbua sana… tunamwomba baba yetu aingilie suala hilo ili tuishi salama kwenye nchi ya watu.

“Tunamwomba kitu kimoja, awe na sisi mkono kwa mkono. Sisi kama kamati ya Wakongo hatuwezi bila kupitia kwake, ubalozi ni baba, kamati ni mtoto,” alisema Lopenge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles