30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Oparesheni ‘mateja’ kutikisa Dar

sirroAsifiwe George na Amani Makala (RCT), Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeandaa oparesheni maalum ya kuwakamata vijana wanaotumia dawa za kulevya maarufu kama ‘mateja’ na wale wanaozurura ovyo mitaani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro alisema oparesheni hiyo itawahusisha wauzaji  na watumiaji wa dawa za kulevya hususan wale wanaojidunga sindano.

Alisema kila mtu atakayekamatwa akiwa ametumia dawa za kulevya atahojiwa na polisi ataje anakozipata.

“Watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wanafahamika, wapo wanaopita bandarini na wanaopita nchi kavu  lakini tunataka tuwakamate na vithibitisho ili tunapowafikisha mahakamani tunakuwa na ushahidi.

“Ni lazima tuwasaidie vijana wetu ambao wanataka kuharibikiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu wanapozurura ovyo nchi yetu ndiyo inayopata aibu,” alisema Kamanda Sirro.

Alisema jeshi hilo halitamwonea haya kijana yeyote  watakayebainika kuuza au kutumia za kulevya na atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles