Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
Serikali imesema haijaweka zuio lolote kwa wasafiri wanaoingia na kutoka nchini, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesena hayo leo Jumatano Mchi 21, wakati alipokuwa akitoa tamko la serikali kuhusu ugonjwa huo.
“Wananchi wasiwe na hofu, serikali tunaendelea kudhibiti na kufuatilia kwa ukaribu mlipuko wa ugonjwa huu, ugonjwa huu hauenezwi kwa kugusana kama inavyodhaniwa bali unaenezwa kwa mbu aina ya Aedes.
“Nasisitiza wananchi wazingatie kusafisha mazingira ili kuua mazalia ya mbu,” amesema.