CARDI B AKANUSHA KUWA MJAMZITO

0
1752


MINNESOTA, MAREKANI
MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Belcalis Almanzar ‘Cardi B’, amekanusha taarifa za kuwa na ujauzito na anatarajia mtoto wa kiume Julai, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mrembo huyo amefunguka na kusema mwili wake unakua kwa haraka na ndiyo maana watu wanadhani kama ana ujauzito.
Taarifa za msanii huyo kuwa na ujauzito zilianza kuenea mara baada ya kufanya tamasha lake la Super Bowl, lililofanyika Minneapolis, Minnesota. Msanii hiyo alionekana akiwa amevaa nguo kubwa, hivyo watu waliamini anazuia kuonekana kwa tumbo lake.
“Nadhani mwili wangu unawatisha watu siku hizi na kuwafanya wajue kuwa nina ujauzito, hakuna ukweli wowote, ninanenepa sana, nadhani itakuwa sababu. Wataendelea kuniona kwenye matamasha mbalimbali hivi karibuni,” alisema Cardi B.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here