31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaipongeza DSTV kwa kukuza tasnia ya sanaa

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dk. Kiango Kilonzo amepongeza Uongozi wa Kampuni ya Dstv Tanzania kwa kukuza tasnia ya sanaa kwa kununua tamthilia mbili kwa mpigo kupitia chanel yao ya Maisha Magic Bongo.

Kampuni hiyo jana imetambulisha Tamthilia mbili za Pazia na Jua Kali ambazo zimesheheni wasanii zaidi ya 100 Mastaa na Chipukizi.

Akizungumza mapema jana wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo, Dk. Kiango amesema serikali inatambua na kuthamini mchango wa Dstv katika kuendeleza tasnia ya filamu.

“Nimekuwa nikiwatembelea wasanii na kujionea uzalishaji wa filamu mbalimbali hapa nchini na nimeridhishwa na kuongezeka kwa ubora na weredi katika uzalishaji wa filamu na maudhui mengi.

“Amewataka wasanii kutumia fursa inayotolewa na Dstv vizuri na kuhakikisha kuwa wanaongeza ubora wa kazi zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje na hivyo tasnia ya filamu kuongeza mchango katika uchumi wa wasanii na taifa kwa ujumla,” amesema Dk. Kioango.

Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema mbali na kutumia wasanii na waigizaji wakongwe wamehakikisha kuwa kuna mchanganyiko wa waigizaji wapya ambao ni vijana.

“Kila mara tunaleta maudhui kulingana na matakwa ya wateja wetu, tunahakikisha kuwa tunawapatia maudhui yanayoboreshwa na yenye vionjo vipaji kila uchao bila kusahau uhalisia wa kitanzania kwenye maudhui yetu,”anasema Shelukindo

Naye, Mwandaaji na Mtunzi wa Tamthilia ya Jua Kali, Lamata Mwendamseke amesema amefurahi kupata nafasi ya pili ya kufanya kazi na kampuni hiyo na kwamba wadau wa sanaa watarajie kuona kazi nzuri yenye uhalisia.

“Hii ni tamthilia ya pili nilianza na Kapuni katika Jua Kali kuna maboresho mengi nashukuru wasanii wametendea haki nafasi zao, nina imani wadau wa Tamthilia na Sanaa kwa ujumla watafurahi,” amesema Lamata.

Kwa upande wa Tamthilia ya Pazia ambayo muandaaji wake ni Samweli Isike amesema katika Tamthilia hiyo ametumia waigizaji wengi vijana ili kuibua vipaji vyao na kukuza.

“Katika Pazia nimeboresha katika uzalishaji, wasanii wengi ni vijana ili kuonyesha uwezo wao kwa sababu wao ndio wanaojenga taifa,” amesem Isike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles