27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Kenya kizimbani kwa kuishi nchini bila kibali

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam

Raia wa Kenya, Brandon Unguko, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana , alikabiliwa na kosa moja la kuishi ndani yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kibaki.

Brandon Unguko, ambaye ni Mkazi wa Mbagala amefikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi mwanndamizi, Rasshidi Chaungu.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali, Khadija Masoud, alidai mtuhumiwa alikutwa Januari 5, mwaka huu katika mtaa wa azikiwe jijini Dar es Salaam

Hata hivyo mtuhumiwa alikana kosa hilo mbele ya Mahakama kutenda kosa hilo, ambapo Wakili Masoud alisema upelelezi umekamilika na kuomba tarehe nyingne kwa ajili ya kusoma hoja za awali.

Naye Hakimu Chaungu amesema kuwa dhamna iko wazi na kutaja masharti ya dhamna ambapo mdhamini mmoja anatakiwa kuwa na barua ya utambulisho iliyoambatanishwa na nakala ya kitambukisho cha uraia na hati ya Sh za kitanzania ya milioni 10.

Hata hivyo mshtakiwa hakufanikiwa kuishi masharti ya dhamna hivyo kurudishwa rumande hadi Januari 13, mwaka huu .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles