32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Morogoro yaamuru mali za Tabora Motel zikamatwe

Na Mwandishi Wetu, Morogoro


Mahakama ya Mwanzo mkoani Morogoro imeamuru vitu mbalimbali ndani ya Tabora Motel iliyopo maeneo ya Nane nane vikamatwe na kukabidhiwa kwa mwenye mali hizo, Denis Msanzya.

Amri hiyo ya Mahakama imetolewa mbele ya Hakimu, Mbawa Daudiosa katika kesi ya madai namba 289 ya mwaka 2019 ambapo mdai ni Mfanyabiashara Msanzya dhidi mdaiwa, Eliminate Komba.

Mahakama hiyo katika Utekelezaji wa hukumu imetoa notisi ya siku 14 kuanzia Desemba 28 mwaka jana kwa Mdaiwa kukabidhi vitu vyenye thamani ya Sh 29,321,000 kwa mdai kwa hiari.

Mahakama hiyo imeamuru kwamba endapo mdaiwa hatatekeleza amri hiyo kwa hiari Utekelezaji utaendelea bila kuarifiwa kwa gharama za mdaiwa.

Iliainishwa kwamba gharama za vitu ambayo ni Sh 29,321,000, malipo ya dalali wa mahakama asilimia kumi Sh 2,932,100, gharama za Utekelezaji Sh milioni moja ambapo jumla Sh 33,253,100.

Mahakama ilifikia hatua hiyo baada ya mdaiwa kukaidi kurejesha vitu hivyo kama alivyoamuliwa na mahakama hiyo katika hukumu iliyosomwa Juni 3, mwaka jana.

Katika hukumu ya Mahakama inasema kwamba mdaiwa akikabidhiwa vitu mbalimbali vya hoteli ya Tabora na bar kwa ajili ya kufanya biashara Januari 20, mwaka jana kwa makubaliano angerejesha ndani ya mwezi mmoja lakini hajafanya hivyo.

“Katika kesi hii hakuna ubishi mdaiwa alikabidhiwa vitu vya hoteli ambavyo walihesabu kwa siku mbili, alivipokea na alisaini kukabidhiwa vitu hivyo kama Elimina Komba.

“Hakuna ubishi hati ya maandishi iliandikwa aliyekabidhiwa ni Elimina Komba na sio Elly Chuma. Mahakama hii imejiridhisha na ushahidi uliotolewa wa pande zote mbili kwamba mdaiwa anatakiwa kurudisha vitu hivyo, mdai ameshinda madai yake , mdai apewe vitu vyake vyote,”ilisema hukumu hiyo.

Baadhi ya vitu hivyo ni samani za ndani ya hoteli hiyo ikiwemo vitanda, meza viti, freezer, feni, magodoro, sofa, televisheni na vingine vyote vikiwa na thamani zaidi ya Sh milioni 29.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles