28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yafunga vituo viwili vya redio

napeeeeNA CHRISTINA GAULUHANGA

-DAR ES SALAAM

SERIKALI imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya redio vya Magic FM cha jijini Dar es Salaam na Redio Five cha jijini Arusha kwa madai ya kukiuka maadili, kanuni za utangazaji na kudaiwa kuleta maudhui ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wa vituo hivyo unakiuka masharti ya kanuni zilizopo.

Alisema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28 (1) cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2013 ameamua kuvifungia vituo hivyo hadi hapo Kamati ya Maudhui itakapokutana na kuwasikiliza kwa kina zaidi na kushauri hatua zaidi za kuchukua kwa mujibu wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005.

“Nimevifungia vituo hivi kwa muda usiojulikana na naieleza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo ili kuwasikiliza kwa kina zaidi na kunishauri hatua za kuchukua ikibidi hata kuvifuta moja kwa moja ama kuwapunguzia adhabu,” alisema Nnauye.

Akitaja sababu zilizosababisha kuvifungia vituo hivyo alisema kipindi cha matukio kilichorushwa Agosti 25, mwaka huu saa mbili usiku hadi saa tatu usiku na kituo cha Utangazaji cha Redio Five cha Arusha kilimhoji Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alielezea mambo mbalimbali ya uchochezi .

“Kwa sababu ya kanuni zetu anayetangaza uchochezi naye pia ni mchochezi, hivyo tumeamua kukifungia kituo hiki huku tukisubiri uamuzi zaidi kutoka Kamati ya Maudhui…kwa sababu maneno yale yalikuwa na nia ya kushinikiza watu wavunje Katiba ya nchi,”alisema Nape.

Kwa upande wa Kituo cha Magic FM, alisema katika  Kipindi cha Morning Magic kipengele cha Kupaka rangi kilichorushwa Agosti 17, mwaka huu kati ya saa moja hadi saa mbili asubuhi, kilikuwa na maudhui ya uchochezi yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani na kukiuka masharti ya kanuni 5 (a), (b), (c) na 18 (1), b (i), (ii) na (iii) ya kanuni za huduma za utangazaji za mwaka 2005.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles