27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yafikia asilimia 64 ya kuwatambua wenye Kifua Kikuu

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MENEJA wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Tanzania, Riziki Kisonga amesema kati ya wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu 95 waliopatiwa matibabu wamepona huku akidai wameweza kufikia uwezo wa kuwatambua wagonjwa kwa asilimia 64 kutoka asilimia 45 mwaka 2015.

Kauli hiyo ameitoa  jana katika uwanja wa  Chinangali Park jijini Dodoma katika banda la Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Tanzania,wakati akizungumza  kwenye maonesho ya Karibu Dodoma Festival ambayo yalikuwa ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu juu ya kazi mbalimbali ambazo zinafanyika ndani ya Serikali.

Wakazi wa Dodoma wakiongozwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima walipata nafasi ya kufika katika banda hilo ambapo huduma mbalimbali za kupima,kupatiwa matibabu na ushauri zilikuwa zikitolewa ambapo pia kulikuwa na gari linalotembea(Kliniki Mobile).

Programu Meneja huyo amesema  Nchi imefanikiwa sana na imeweza kuwafikia uwezo wa kuwatambua wagonjwa kwa asilimia 64 kutoka asilimia 45 mwaka 2015 ambapo amedai hayo ni mafaniko makubwa.

Amesema katika hali ya kawaida mgonjwa mmoja wa TB ambaye anamakohozi yenye wadudu asipo tibiwa anaweza kuambukiza watu wengine 10 mpaka 20 kwa mwaka hivyo tatizo likaendelea kuongezeka.

Kisonga amesema mpango huu ulianza mwaka 1977 ukiwa na lengo kubwa la kuhakikisha kwamba ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma vinatokomezwa nchini.

Amesema malengo makubwa ya mpango ni kuhakikisha wanapunguza idadi ya wagonjwa wanaopata TB nchini kwa asilimia 50 lakini tuna taka kupunguza vifo vya wagonjwa kwa asilimia 35 na kutokomeza kabisa ukoma katika nchi hii ifikapo mwaka 1930

Amesema katika dunia kuna idadi kubwa  ya wagonjwa wanaofika milioni 8 mpaka 10 na kati ya hao dunia inauwezo wa kuwatambua wagonjwa milioni saba ambapo amedai maana yake kuna asilimia kubwa ya wagonjwa bado hatujawafikia.

“Inakadiriwa kwa mwaka 2020 tulikuwa na wagonjwa wapatao 133,000 ni kutokana na takwimu zinapokatikana nchini kwetu na kati ya wagonjwa hao nchi iliweza kuwafikia wagonjwa 85 kwa kuwatambua kwamba wanaugonjwa wa Kifua Kikuu na kuwaweka katika matibabu.

“Lakini wote waliowekwa katika matibabu matokeo ya tiba ni makubwa na mazuri tumefikia asilimia 95 kwa lugha nyingine tuseme kati ya wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu  wagonjwa 95 wanapona wengine wanaweza kupata matatizo mbalimbali kutokana na kutokutumia dawa.

“Wito wetu mkubwa ni kuhakikisha jamii inatambua kwamba kifua Kikuu kipo na dalili zake zipo mtu anakohoa kikohozi hata ukitibiwa na dawa zingine unaona kinaendelea tu ni vizuri tukaenda kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi,”amesema Kisonga.

Amesema dalili zingine ni  wakati wa baridi mtu kutoka jasho na wakati mwingine kuumwa kifua Kikuu kinaathiri sehemu yote ya mwili isipokuwa kucha na nywele.

“Tuna Kliniki tano kama hizi ambazo zimenunuliwa na Serikali ambazo zimewekwa katika Kanda tano,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles