26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yafafanua tuzo ya Lulu

LuluNA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefafanua kwamba filamu ya ‘Mapenzi ya Mungu’ ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos, Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA), aliipata kwa kuwa yeye ndiye mmiliki wa filamu hiyo.

Taarifa kutoka wizara hiyo zimeeleza kwamba, filamu hiyo imetengenezwa chini ya Kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190 na Lulu ndiye mwenye haki zote za umiliki wa filamu hiyo ndiyo maana alipata tuzo hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba, ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo, muswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles