23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaendelea kuhimiza wananchi uwekaji Anuani za makazi

Na Mwandishi Wetu, Lindi

Naibu Katibu Mkuu, Kaspar Mmuya amehimiza wananchi ambao bado maeneo yao hayajatambuliwa kwenye zoezi uwekaji anwani za makazi kujitokeza kwenye Ofisi za serikali za Mitaa au Kijiji kueleza ili uongozi uwawekee namba.

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akizungumza katika ziara yake ya kukagua zoezi la uwekaji wa anwani za makazi Mkoani Lindi alipotembelea Halmashauri ya Mtama na Manispaa ya Lindi.

Amezungumza hayo Mei 16, 2022 katika ziara yake ya kikazi Mkoa wa Lindi alipotembelea kujionea utekelezaji wa zoezi la anwani na makazi ambalo limeweza kutambua barabara na mitaa 7,972 na majengo na viwanja 334,771 vimeweza kutambuliwa na kuingizwa kwenye mfumo wa NAPA.

“Mkoa wa Lindi umefaulu vizuri sana katika kuweka miundo mbinu hasa ya barabara na wamefanikiwa vizuri kuyatambua maeneo yake na kuyapa namba ikiwa inamaanisha nyumba na barabara nyingi kutambuliwa kwa majina alisema Naibu Katibu Mkuu,“ amesema Mmuya.

Ameongeza kuwa mitaa ambayo haijabandikwa kibao na jina imepewa mpango kazi na miundo mbinu inatengenezwa kwa kushirikiana vizuri na TANROAD pamoja TARURA katika barabara zinazohusu taasisi zetu hizi mbili. 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akiangalia Ubunifu wa kupaka rangi na kuandika postikodi kwenye nyumba katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa anwani za makazi katika Mkoa wa Lindi.

Amefafanua zaidi kuwa uelewa wa wananchi katika kulipokea na kulitekeleza jambo hili ni mkubwa kwa sababu wameshirkishwa katika kutafuta majina hayo ya mitaa na wanajua umuhimu wa kuwepo kwa miundo mbinu hiyo.

“Wananchi walio wengi wamekubali kuzichora nyumba zao kwa kutumia rangi ya njano na kuweka namba katika nyumba kwa kutumia rangi nyeusi, ni wajibu wetu kama kanuni za anwani za makazi ambazo zimewekwa na TAMISEMI kanuni namba 20 ambayo inasema ni wajibu wa mwenye nyumba kuweka namba hiyo kwenye nyumba yake,” amesema Mmuya.

Akihitimisha Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Lindi, Injinia Dawson Paschal amesema watawekwa nguzo na vibao 3,042 katika Mkoa mzima wa Lindi. Vibao vitakavyotengenezwa vitafidia sehemu ambazo hazijawekwa ili kuhakikisha zoezi la uwekaji wa miundo mbinu linafanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles