27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Hoseah ajivunia wananchi kupata msaada wa kisheria bure, kudhibiti Mawakili feki

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kinatarajia kufanya uchaguzi Mkuu katika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais na Mweka hazina.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu jijini Arusha, ambapo tayari kamopeni za wagombea urais zimeanza tangu Aprili 15 na zinatarajiwa kuhitimishwa Mei 26, mwaka huu siku ambayo pia utafanyika uchaguzi katika nafasi nyingine ukiwamo ya viongozi wa kanda.

Mgombea wa nafasi ya Urais katika Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Profesa Edward Hoseah.

Uchaguzi huo ni kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ambao hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.

Miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais ni Profesa Edward Hoseah ambaye anawania nafasi hiyo kwa awamu ya pili.

Prof. Hoseah anaomba nafasi hiyo kwa mara nyingine kwa kile anachoamini kuwa ameweza kutekeleza vyema majukumu yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Katika mahojiano maalum na Mtanzania Digital, Prof. Hoseah anasema pamoja na mambo mengine chini ya uongozi wake wamefanikiwa kuishauri Serikali kufungua kituo cha kimataifa cha utatuzi wa migogo ya kibiashara na kutoa msaada kwa wananchi.

“Tumeweza kuishauri Serikali kufungua kituo cha Kimataifa hapa nchini kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara (Tanzania International Arbitration Centre) ili kuepukana na adha ya kwenda nje kutatua migogoro kwani ni gharama kubwa.

“TLS imekuwa ikitoa msaada wa kisheria bure kwa Wananchi ambao hawana fedha ya kupata huduma ya kisheria, ili kuwawezesha wananchi kupata haki na stahili zao,” anasema Prof. Hoseah.

Anasema kuwa TLS wamekuwa sehemu ya washiriki katika kikosi kazi cha kukusanya maoni ya katiba.

“Moja ya mambo yanayotazamiwa ni suala la katiba mpya TLS, tunashiriki kikamilifu katika kikosi kazi kilichoundwa kukusanya maoni na nyaraka zitakazosaidia kutoa dira ya namna gani tunakwenda katika mchakato wa katiba mpya.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wangu TLS imeweza kushauri zile sheria kandamizi kuondolewa au kurekebishwa ili kuimarisha misingi ya utoaji haki nchini kwa maslahi mapana ya wananchi na ustawi wa Taifa letu.

“Ndani ya Mwaka mmoja wa uongozi wangu ndani ya TLS tumejitahidi kujenga mahusiano mazuri kati ya mihimili ya kiserikali na Mawakili ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakihisi tofauti,” anasema Prof. Hoseah.

Anaongeza kuwa: “Uongozi wa TLS kwa kushirikiana na serikali tumeweza kupunguza gharama za bima ya afya kwa Mawakili kutoka Milioni 1 hadi 500,000.

“Kipindi cha nyuma kulikuwa na ongezeko kubwa la Mawakili feki (vishoka) lakini kwasasa tunakwenda kudhibiti hilo kwani Mei 22, kwenye mkutano wa wanasheria tunakwenda kuzindua mihuri ya moto (Digital stamps) kwa ajili ya kuzuia mihuri na Mawakili feki mtaani,” anasema Prof. Hoseah.

Usikose kusoma mwendelezo wa mahojiano haya hapa na kwenye mitandao yetu ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles