25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAAGIZA MRADI REAIII KUANZA MWEZI HUU

Na Mwandishi Wetu, Mbeya


SERIKALI imeagiza utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), uanze mwezi huu sambamba na utekelezaji wa Mradi wa Densification ambao upo kwenye utekelezaji.

Naibu Waziri Nishati, Subira Mgalu,alitoa agizo hilo, wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo Mradi wa Umeme Vijijini unatekelezwa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.

Akizungumzia na baadhi ya wananchi Wilayani humo ambao walimueleza kero mbalimbali zinazohusu masuala ya Nishati ya Umeme ambayo ni kukatika kwa umeme mara kwa mara bila taarifa, kucheleweshwa kuunganishwa na huduma ya umeme kwa ambao tayari wamelipia, baadhi ya Taasisi (shule, zahanati, vituo vya afya na visima vya maji) kurukwa wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II).

Baada ya kuzungumza na wananchi hao kwa nyakati tofauti, akijibu kero zao, Naibu Waziri Mgalu aliagiza Mradi wa REA III uanze kutekelezwa ndani ya Mwezi huu wa januari, 2018 bila kuchelewa.

“Utekelezaji wa Mradi wa Densification ambao unafanyika hivi sasa, uende sambamba na utekelezaji wa Mradi wa REA III kuanzia Mwezi huu wa Januari, 2018,” aliagiza Mgalu.

Akizungumzia suala la kucheleweshwa kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi waliolipia, Mgalu aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wateja wote waliolipia umeme wanaunganishwa mara moja bila kuwepo visingizio.

“Tulikwisha agiza maombi yote ya wateja kuunganishiwa umeme yatekelezwe ndani ya Siku Saba baada ya kulipia,” alisema Naibu Waziri Mgalu.

Kuhusu suala la baadhi ya maeneo kurukwa hususan maeneo ya huduma za kijamii zikiwemo shule, zahanati, vituo vya afya na visima vya maji, Naibu Waziri Mgalu alisisitiza kwamba wakati wa utekelezaji wa Mradi huo wa REA III, maeneo hayo yapewe kipaumbele.

“Tunakiri utekelezaji wa REA II, ulikuwa na mapungufu ikiwemo ya kuruka baadhi ya maeneo, ninawahakikishia kasoro hii haitojirudia kwenye REA III,” alisema.

Baadhi ya maeneo ulikopita,wilayani Kyela ni Bandari ya Itungi; Kata ya Kajunjumele; Kata ya Nkuyu; Kata ya Ibanda na Kata ya Kasumulu.

Waziri Mgalu yupo mkoani Mbeya kwa ajili ya ziara ya kukagua utekelezaji  Miradi ya Umeme Vijijini na Miradi mingine ya umeme Mkoani humo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles