24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

KIFO CHA MFUNGWA CHAIBUA MGOGORO MISRI

CAIRO, Misri


MAPIGANO yameripotiwa kati ya vikosi vya polisi na waandamanaji nje ya kituo cha polisi mjini Cairo kutokana na kifo cha kijana mmoja aliyekuwa rumande.

Taarifa zinasema kuwa waandamanaji hao wanaishutumu polisi kwa kumtesa mpaka kumsababisha kifo kijana huyo.

Pamoja na vurugu nyingine, walichoma magari ya polisi, kuyapiga mawe na kujaribu kuchoma pia kituo cha polisi.

Aidha, Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na kuwakamata baadhi ya waandamanaji.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Afroto,s alikamatwa siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya na polisi walisema alifariki baada ya kupigana na wafungwa wenzake.

Hali ya utulivu ilirejea katika Mji wa Cairo baada ya Mkuu wa Polisi kuahidi kufanya upelelezi wa suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles