23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutumia watu mashuhuri duniani kuchangisha fedha mapambano ya Ukimwi

Upendo Mosha – Hai

Swerikali imeanza mkakati wa kuhamasisha watu mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wanasiasa pamoja na wasanii ili kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwaajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala ameyasema hayo leo Juni 15, wakati akizindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro la watu 80 kutoka nchi mbalimbali duniani la kuchangisha fedha za mapambano  dhidi ya Ukimwi, kampeni ambayo imendaliwa na mgodi  wa Madini ya Dhahabu ya Geita (GGM).

Amesema wizara ya Maliasili na Utalii itaanda utaratibu wa kuhamasisha makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wasanii na watu mashuhuri duniani kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi kwani mapambano ya virusi hivyo ni ya watu wote na sio ya serikali pekee.

Waziri Kigwangala amesema takwimu za maambukizi mapya hususan katika kundi la vijana yanatisha na kwamba zinahitajika jitihada za makusudi kutoka Katika kundi hilo kudhibiti ugonjwa huo.

“Hali ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yanatisha ni lazima sisi Kama vijana  tuwe msitari wa mbele kupambana na Hali hii, kwa mwaka nimepanga kupanda Mlima huu na watu mashuhuri ikiwemo wanasiasa na wasanii ili kuchangisha fedha kwaajili ya kudhibiti ugonjwa huu”amesema

Akizungumza, Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchi (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko, amesema kila siku watu zaidi ya 200 huambukizwa virusi vya ukimwi ambapo Kati yao asilimia 80 ni vijana kwanzia miaka 15-24.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Richard Jordinson, amesema tangu kampeni hiyo kuanzishwa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi billion 13 na kwamba katika kampeni ya mwaka huu nchi zaidi ya 72 zimeshiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles