30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mikoa nane yapewa mwaka kukamilisha Mwongozo wa uwekezaji.

Mwandishi wetu – Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga kuhakikisha imekamilisha kuandaa Mwongozo wa uwekezaji.

Ametoa maagizo hayo leo Juni 15, alipokuwa akifungua Kongamano la nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kauli mbiu yake ni wezesha watanzania Kujenga viwanda.

Majaliwa ameitaka mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao.

Aidha ameitaka NEEC Kuendelea kuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2015 hadi 2020 kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.

“Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iboreshwe sambamba na kuongeza ufanisi ili iweze kuwafikia Watanzania wengi hususan wale wa vijijini, vilevile kamilisheni na hakikisheni mnazindua haraka mfumo wa kupima mifuko ya uwezeshaji kwa matokeo ya kiuchumi na kijamii na siyo kwa shughuli walizofanya.” amesema.

Ameongeza kuwa uwezeshaji wananchi kiuchumi ni suala mtambuka na kwamba sekta mbalimbali za kiuchumi na sekta binafsi zinajihusisha moja kwa moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, hivyo ni muhimu masuala ya uratibu, ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi, yakafanywa mara kwa mara ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles