Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital
SERIKALI imesema itahakikisha inaondoa vikwazo vya kiuchumi vinavyosababisha Wafanyabiashara wanaotoka nje ya nchi na kuingia hususan mipakani wanafanya shughuli zao bila kubughudhiwa.
Akizungumza leo Agosti 16, 2022 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Ripoti ya Wafanyabiashara wa mipakani iliyoratibiwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Liberty Sparks, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigae amesema hadi sasa tayari vikwazo 30 vya kibiashara vimeshaondolewa.
Amesema ripoti iliyoandaliwa na Siberty spark ni muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.
“Serikali inampango wa kuweka sehemu moja taasisi zote zinazohusiana na biashara ili kumrahisishia mfanyabiashara kuweza kufanya shughuli za kibiashara kwa muda mfupi,”amesema Kihega.
Amesema ili kusajili kampuni ya biashara zamani ilikuwa lazima ipite miezi mitatu ndio ufanikishe lakini kwa sasa kampuni itasajiliwa ndani ya wiki moja.
“Serikali ya awamu ya sita ni serikali sikivu kwa sababu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amewapa kipaumbele wafanyabiashara,” amesema.