24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kukagua dawa kuanzia bandari

ummyNa Bakari Kimwanga, Dodoma

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetangaza mkakati wa   ukaguzi wa dawa    zinapoingia katika Bandari ya Dar es Salaam  ikiwa ni mkakati wa kuzuia upotevu.

Imesema   imeandaa mpango unaojulikana kama ‘Pilferage Tool’ ambao utatumika   kufanya ukaguzi wa upotevu wa dawa unaosadikia kutokea kuanzia mzigo unapoingia bandarini mpaka kumfikia mgonjwa.

Mkakati huo ulitangazwa jana bungeni mjini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alipowasilisha bajeti ya wizara yake ya Sh bilioni 277.6.

Alisema   mfumo huo utasaidia upatikaji wa dawa kwa hospitali zote nchini.

Waziri alisema pia kuwa  Serikali imefanya mapitio ya kina  ya mfumo wa ununuzi na utunzaji wa dawa  katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

“Ili kuepuka kulipa kodi na tozo zilizo juu kutokana na misaada inayoletwa nchini bila kuwa na utaratibu maalumu wa kupokea misaada hiyo.

“Wizara itatoa mafunzo ya kusambaza na kusimamia utekelezaji wa mwongozo wa ufanisi wa kazi kupitia mfumo wa 5S Kaizen TQM   kuimarisha usimamizi wa takwimu za dawa,” alisema Ummy.

Alisema wizara   imeendelea kuboresha huduma ya afya ya uzazi na motto na  katika mwaka 2015/16   iliwajengea uwezo watoa huduma jinsi ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa na upungufu wa uzito.

Licha ya hali hiyo suala la vifo vinavyotokana na uzazi bado ni changamoto  ambako kutokana na taarifa za Umoja wa Mataifa (UN),    Tanzania imepunguza vifo hivyo kutoka 454 mwaka 2010 hadi 398 mwaka 2015.

“Ili kuhakikisha vifo hivi vinaendelea kupungua kwa kasi zaidi wizara imehakikisha  watoa huduma wa afya 2,087 wamejengewa uwezo kwa kuwapatia mafunzo ya huduma muhimu wakati wa ujauzito, stadi za kuokoa maisha kwa matatizo ya dharura yatokanayo na mtoto mchanga na baada ya kujifungua,” alisema.

Akizungumzia huduma za chanjo, alisema  wizara itaendelea kutoa miongozo ya huduma za chanjo kulingana na miongozo.

“Pia Wizara imeendelea na juhudi za kudhibiti UKIMWI kwa kutoa ushauri nasaha na kupima na kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana,   wateja wapya 3,474,780 walipata ushauri nasaha na kupima VVU.

“Na idadi hii inajumulisha pia waliopata huduma kupitia mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto PMTCT,”  alisema.

 

Maoni ya upinzani

Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Msemaji wa  Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Godwin Mollel, alisema   suala la upungufu wa madawa unaweza kuongezeka kwani Serikali imetenga Sh bilioni 65.1 kwa ajili ya ununuzi wa dawa.

Alisema kiasi hicho kinatosha mahitaji ya nchi kwa mwezi mmoja na nusu tu kwa   kukadiria kuwa Tanzania ina watu takribani milioni 49.8  wanaohitaji matibabu, kiasi kilichotengwa kinatosha kutibu watu milioni 5.6 kwa mwaka.

“Je, watu wengine milioni 44 wanaobaki watatibiwa na nini na wapi? Mheshimiwa Spika: Kambi Rasmi ya Upinzani inaishauri Serikali iongeze bajeti ya madawa kutoka asilimia 11 (bilioni 65.1) mpaka angalau asilimia 50 ya mahitaji  (bilioni 295.9).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles